MHASHAMU Askofu mkuu wa Jimbo la Shinyanga Kanisa katoliki amefariki
dunia akiwa katika hospitali ya rufaa ya Bugando alikokuwa akitibiwa.
Historia yake:
Mhashamu Askofu Aloysius Balina alizaliwa Juni 21, 1945
katika kijiji cha Isoso Ntuzu wilayani Bariadi mkoani Shinyanga na aliwekwa wakfu na Papa
Yohane Paulo II mwaka 1984 kuwa Askofu wa Geita na kusimikwa Machi 10, 1985.
Septemba 23, 1997 alihamishiwa Jimbo la Shinyanga na kuwa
Akofu wa tatu wa Jimbo la Shinyanga hadi mauti yalipomkuta, huku watangulizi
wake wakiwa Askofu Edward A. McGurkin, aliyetumikia cheo hicho toka mwaka 1956
hadi 1975, alifariki Agost 281983 huko Marekani, wa pili ni Askofu Castor
Sekwa, aliyetumikiwa kuaznia mwaka 1975 hadi Juzi
6, 1996 alippofariki na askofu Balina kushika nafasi yake.
Taarifa kamili zitatolewa
0 comments:
Post a Comment