CHAMA Cha
Mapinduzi wilayani Kahama kimewaagiza viongozi wa serikali wa kata ya Mapamba
kuhakikisha wanasimamia upatikanaji wa fedha zaidi ya Shilingi Laki Tisa
zilizopotea ambazo zilikuwa zimechangwa na wananchi kwa ajili ya Ujenzi wa
shule ya Sekondari,katika Kata hiyo.
Agizo hili limetolewa
jana na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kahama,Mabala Mlolwa baada ya kuelezwa kuwa
ujenzi wa shule hiyo ya sekondari umekwama kutokana na wananchi kugoma kuchanga
baada ya fedha za Awali kutokujulikana zilipo.
Kufuatia hali hiyo
bwana Mlolwa amewapa majuma matatu kuhakikisha mapato na matumizi ya fedha hizo
yanasomwa na fedha zinazodaiwa kupotea zinajulikana zilipo ili ujenzi wa shule
hiyo ya Sekondari unaendelea.
Kabla ya hapo Katibu
wa UChumi na fedha wa Chama hicho wilaya ya Kaham,Isaya Bukakiye,aliwataka
viongozi wakiwemo mabarozi wa chama hicho kuhakikisha wanakuwa mstari wa mbele
kusimamia maendeleo ya wananchi hali itakayo kijenga chama.
Ili kuboresha
shughuli zao za Chama;Bwana Bukakiye aliahidi kuwapatia baiskeli mabalozi wote
wa wilaya ya Kahama,ili waweze kufanya kazi zao kwa urahisi zaidi ili
waondokane na hali ya ,madai ya kutumika kwenye Chama wakati wa uchaguzi pekee
na ukiisha wanasahaulika.
0 comments:
Post a Comment