Home » » VIBAKA WAUA TRAFIKI

VIBAKA WAUA TRAFIKI

WATU wanaodhaniwa kuwa ni vibaka kutoka katika machimbo ya dhahabu ya Nyangarata na Mwime wilayani Kahama mkoani Shinyanga,ambayo yamekwisha uzalishaji wake,wamemuua askari wa Usalama barabarani;Salum Mtepa mwenye cheo cha Staff Sajenti,kwa kumpiga na kitu kizito kifuani.

Tukio hilo limetokea nyumbani kwake eneo la Majengo mjini Kahama usiku wa kuamkia leo baada ya watu hao wanaokadiriwa kuwa wanne kufika nyumbani kwake na kuvunja kibanda cha biashara kwa lengo la kuiba ndipo askari huyo alipotoka nje kwenda kupambana nao.
 

Kwa mujibu wa taarifa ya Mkuu wa Polisi wilaya ya Kahama George Simba,askari huyo alipigwa na kifaa hicho kifuani wakati akijaribu kupambana na vibaka hao,hali iliyopelekea kuvuja damu nyingi ndani ya kifua na kusababisha kifo chake.

Simba amesema hali ya vibaka katika mji wa Kahama ni mbaya kwani wameongezeka kutokana na machimbo ya Nyangarata kujaa maji na Mwime kuisha uzalishaji wake,hali iliyofanya vijana wengi kutoka kwenye maeneo hayo bila kuwa na fedha.

Amesema hivi sasa wimbi la vibaka hao limekuwa tishio huku akiahidi kupambana nao ikiwa ni pamoja na kuwasaka kwa nguvu zote vibaka waliohusika na kifo cha askari huyo wa usalama barabarani,ingawa hadi jana hakuna mtu yeyote aliyekuwa amekamatwa juu ya kuhusika na tukio hilo.

0 comments:

 
Supported by Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Shinyanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa