Home » » JESHI WATOA MSAADA KWA WALEMAVU

JESHI WATOA MSAADA KWA WALEMAVU


Shinyanga
Wakati leo ikiwa siku ya majeshi Tanzania vikosi vya jeshi hilo mkoani Shinyanga vimetoa msaada wa vyakula katika kituo cha walemavu wa ngozi Albino cha Buhangija kilichopo mansapaa ya Shinyanga kinachokabiliwa na janga la njaa.
Kamanda wa vikosi hivyo mkoani Shinyanga Kanal Emanuel Mbonile Amesema msaada huo wa chakula ambachi ni mchele,unga na mafuta pamoja na sabuni vinathamani ya zaidi ya shilingi milioni moja.
amesema jeshi limeambua kutoa msaada huo ikiwa ni sehemu ya kuazimisha miaka 49 pamoja na kusaidia  kituo hicho ambacho kwa sasa kinakabiliwa na taitzo la chakula
hata hivyo Mbonile ametoa wito kwa wasamalia wengine kukisaidia kituo hico chenye watoto wenye ulemavu zaidi ya 250
awali mkuu wa kituo hicho mwalimu Peter Ajari amelishukuru jeshi kwa msaada wa chakula hicho ambacho kitasaidia kupunguza makali ya njaa kwa zaidi ya wiki moja
amesema kituo chake kwa sasa kinakabiliwa na upungufu wa chakula na kuwaomba wasamalia wema kujitokeza kutoa misaada yao

0 comments:

 
Supported by Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Shinyanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa