Katibu
Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahaman Kinana septemba 10
anatarajiwa kuanza ziara ya kawaida katika mikoa ya Shinyanga, Simiyu na
Mara.
Ziara
hiyo itaanzia katika mkoa wa Shinyanga septemba 10 mpaka 13 mwaka huu,
kwa kutembelea wilaya zote nne za mkoa huo na kufuatiwa na mkoa mpya wa
Simiyu kuanzia Septemba 14 mpaka septemba 19 kwa kutembelea wilaya zote
tano Kabla ya kuhitimisha ziara hiyo kwa kutembelea wilaya Sita za mkoa
wa Mara kuanzia Septemba 20 Mpaka 25 mwaka huu.
Katika
ziara hiyo Katibu Mkuu wa CCM ataambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu
ya Taifa ya CCM anayeshughulikia Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye.
Kwa
mujibu wa Ratiba ya ziara hiyo, Wajumbe hao wa sekretarieti watakagua
uhai wa Chama ikiwa ni pamoja na kupokea wanachama wapya sanjari na
kuhamasisha wananchi kujituma katika shughuli za uzalishaji ili Kuleta
tija katika maisha Yao na ya taifa kwa ujumla.
Aidha
watakagua maendeleo ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka
2010/2015 hasa katika miradi ya kimaendeleo Kama vile Ujenzi wa majosho
kwa ajili ya wafugaji, maendeleo ya maboresho ya kilimo cha Pamba,
uvuvi wenye tija pamoja na maboresho ya sekta za Afya, elimu na
miundombinu zikiwemo Barabara.
Katika
ziara hiyo Katibu Mkuu atapata fursa ya kusikiliza kero mbalimbali za
wananchi na kwa kushauriana na serikali kutafuta namna ya kuzitafutia
ufumbuzi.Katibu mkuu pia atafanya mikutano ya ndani, na ya hadhara
katika kila wilaya za mikoa hiyo.
Imetolewa na;
Nape Moses Nnauye
Katibu wa Itikadi na Uenezi
05/09/2013
0 comments:
Post a Comment