MGODI wa dhahabu wa Bulyanhulu
unaomilikiwa na Kampuni ya African Barrick Gold Mines Ltd, unatarajia kulipa
kiasi cha Shilingi Bilioni 1,250 kwa wakazi wa Kijiji cha Kakola namba Tisa
waliopisha mgodi huo kuongeza eneo la uwekezaji.
Mkuu wa wilaya ya Kahama;Bwana
Bensoni Mpesya,amesema hayo juzi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji
hicho kilichopo kata ya Bulyanhulu,ambapo kiasi hicho ni kwa ajili
ya wakazi 143 ambao wameridhia kuacha maeneo na mashamba yao ili kampuni
hiyo iongeze eneo la uchimbaji madini.
Bwana Mpesya amesema kiasi hicho cha
fedha ni pamoja na faini ya asilimia nane ambazo Serikali ya wilaya iliafikiana
na mgodi uwafidie wakazi hao kutokana na kuwacheleweshea stahiki zao.
Hivi karibuni baadhi ya wakazi hao
walizuia upanuzi wa ujenzi wa uzio wa Mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu katika
Kijiji cha Namba Tisa, katika maeneo waliyompisha Mwekezajni
huyo,kutokana na kucheleweshewa malipo hayo, ambapo mgogoro huo umetatuliwa na
Mkuu wa wilaya ya Kahama.
0 comments:
Post a Comment