Watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino)
Madaktari hao pia watatembelea kituo cha watoto yatima cha Chakuhama eneo la Sinza jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuchunguza afya zao na kuwapa misaada ya matibabu.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mke wa Balozi wa Uturuki, Yesim Davutoglu, wakati akikabidhi baiskeli za watu wenye ulemavu 10 kwa ajili ya kuwasaidia usafiri pale wanapotoka katika kazi zao, alisema ujio huo utakuwa chini yake kupitia Ubalozi wa Uturuki uliopo nchini.
Davutoglu alisema ameamua kutoa msaada huo ili kuwanasua na hali ngumu ya maisha hasa tatizo la usafiri.
Alisema baada ya kutoa baiskeli hizo, anatarajia kutoa nyingine 10 baada ya siku 15, kwa walemavu wengine ambao nao walikuwapo katika orodha ya wale aliopanga kuwapa msaada. Davutoglu alisema zoezi hilo amekuwa akilifanya katika nchi mbalimbali alizoishi kwa kusaidiwa na wafanya biashara wakubwa kutoka nchini Uturuki.
Alisema anatarajia kujenga kituo cha watoto Albino jijini Dar es Salaam, ambacho kitasaidia kuwaweka pamoja ili kuwapa misaada mbalimbali wanayohitaji kama jamii nyingine.
Alisema amepanga kufanya hivyo ili kutoa urahisi kwa jamii hiyo kupata misaada kutoka kwake na watu wengine ambao wataguswa na kile atakachokifanya kwa ajili ya kuendeleza Albino waliopo katika sehemu tofauti hapa nchini.
Alisema amefikia hatua hiyo, baada ya kupita katika Mkoa wa Shinyanga na kukuta albino wengi, wakiwa sehemu moja na kuvutiwa kufanya hivyo jijini Dar es Salaam, ili kuletaurahisi kutoa misaada pale anapohitajika.
Aliiomba serikali kumsaidia ili zoezi hilo lifanikiwe kwa imani kuwa litakuwa zuri kwa jamii ya watu hao ambao wamekuwa wakihangaika kutokana na wengi wao kukosa misaada pale wanapohitaji.
CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment