Njozi
njema ya wakazi wa kijiji cha Bulekela, kata ya Masanga wilayani
Kishapu ya kupata maji safi na salama kwa mtandao wa bomba imepotea
baada ya mradi huo kabadilishwa kinyemela kuwa wa pampu ya kusukuma
kwa mkono.
Baadhi
ya wananchi wakiwemo wajumbe wa kamati ya mradi wa ujenzi wa mtandao
huo wamemlalamikia Mkurugenzi wa halmashauri hiyo kwa kubadili hali
ya mradi huo ambao ungefikia vitongoji (7) vya kijiji hicho kuwa wa
kile wanachodai 'tologo'
mhasibu
wa kamati ya mradi huo, Martha Elias akizungumza kwa njia ya simu
amesema kuwa mtaalamu aliyesimamia uchimbaji wa visima virefu (2)
vya mradi huo Bw. Mbaga, aliwathibitishia wananchi kuwa maji ya
kutosha yalikuwa yamepatikana.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kata ya Masanga, John Gamaya amesema mradi huo wa mtandao wa bomba katika vitongoji vyote (7) ulipangwa kutumia takriban shilingi 328m zilizotolewa ufadhili na benki ya Dunia.
Aidha wakazi hao wa Bulekela wanadai kuwa kuweka pampya kusukuma kwa mkono kwenye visima hivyo wanawake na watoto watahatarisha maisha yao kwa kulazimika kuvuka mto Tungu kwenda kuchota maji kwenye visima hivyo ng'ambo ya mto huo.
Alipotafutwa ili kuzungumzia mgogoro huo, Mkurugenzi Mtendaji alidai kuwa kwenye mkutano na alipopigiwa baadaye hakupokea simu siku nzima.
0 comments:
Post a Comment