Home » » SIKU YA KISUKARI MKOANI SHINYANGA

SIKU YA KISUKARI MKOANI SHINYANGA


1 -3. Siku ya Kisukari iliyofanyika jana duniani kote,mkoani Shinyanga ilifanyika katika Manispaa ya Shinyanga kwa matembezi yaliiongozwa na Mkuu wa Mkoa Mhe.Ally N.Rufunga(mwenye "track suit" nyeusi),Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Dkt.Anselm Tarimo,Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Ramadhani Kabala,Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe.Anna Rose Nyamubi na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama,watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa,wanafunzi wa Shule za msingi na Sekondari na wananchi.

2. Matembezi hayo yalianzia hospitali ya mkoa wa Shinyanga na kumalizia uwanja wa "Shycom", lengo likiwa kutoa ujumbe kwa wananchi kujikinga na ugonjwa wa kisukari kwa kubadili mtindo wa maisha na tabia ya ulaji.

4. Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe.Ally N.Rufunga akizungumza na wakazi wa Shinyanga katika maadhimisho ya siku ya Kisukari yaliyofanyika jana katika viwanja vya Shycom katika Manispaa ya Shinyanga.

Na Magdalena Nkulu
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Shinyanga

0 comments:

 
Supported by Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Shinyanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa