Shinyanga.Naibu Katibu wa Chadema, Zitto Kabwe
amewataka wakazi wa Manispaa ya Shinyanga wawachague viongozi wanaofanya
siasa za vitendo na siyo maneno.
Alisema hayo jana wakati akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika Viwanja vya Mahakama ya Mwazo mjini humo.
Alisema wananchi wanatakiwa kuamka kwa kuwatathimini viongozi waliowachagua katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.
Zitto alisema siasa za maneno zilishapitwa na
wakati na kwamba siasa iliyo bora ni ya vitendo kwa maana ya kuwaletea
wananchi maendeleo.
‘Siasa za maneno zilishapitwa na wakati sasa hivi
siasa ni vitendo tu maana wananchi wameshachoshwa na ahadi za viongozi,”
alisema Zitto
Katika hatua nyingine mbunge huyo wa Kigoma
Kaskazini, alisema amekuwa akisafiri kwenda nje ya nchi kufuatilia fedha
zilizofichwa na kampuni za wafanyabiashara wakiongozwa na baadhi ya
viongozi wakubwa serikalini.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment