Naibu Waziri wa Maji,Dk. Binilith Mahenge
Naibu Waziri wa Maji, Dk. Binilith Mahenge, aliliambia Bunge jana kuwa fedha hizo ni kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maji vijijini.
Mahenge alisema katika mpango huo, pia kutakuwa Sh. milioni 508.5 kupitia mfuko wa pamoja na Sh. 358.7 kupitia ongezeko la mgawo wa fedha za ndani.
Alisema katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, serikali inatekeleza mradi wa vijiji 10 kati ya vijiji 15 ambavyo vilibainishwa kuwa na matatizo makubwa ya maji.
Hata hivyo, alikiri kuwa fedha zinazopelekwa katika miradi ya maji vijijini zimekuwa zikichelewa kufika katika maeneo husika na kusababisha kazi hizo kuchelewa.
Kwa mujibu na Naibu Waziri, vijiji vitakavyonufaika na miradi hiyo ni Sanyu, Bunongwa, Kazuni, Mishepo, Didia, Mendo, Nyashimbi na Manyanda.
Vingine ni Mwamadilanha na Mwakitolyo ambavyo vyote shughuli zake zipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji wakati vijiji vya Sanyu na Bunonga vimekamilika.
Mahenge alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Azzan Hamad (CCM), aliyetaka kujua kiasi cha fedha kilichotengwa kwa ajili ya kutatua tatizo la maji lililopo Halmashauri ya Shinyanga.
Pia, alitaka kufahamu idadi ya vijiji vitakavyonufaika na ongezeko hilo kwani wananchi wamekuwa wakipata adha kubwa ya kupata maji katika maeneo yao.
CHANZO:
THE GUARDIAN
0 comments:
Post a Comment