Home » » MSALALA WAANZA KUJENGA VYOO VYA SHULE YA MSINGI BUGARAMA

MSALALA WAANZA KUJENGA VYOO VYA SHULE YA MSINGI BUGARAMA

HALMASHAURI ya Msalala wilayani Kahama imeanza kuvijenga vyoo matundu 20 kwenye Shule ya Msingi Bugarama iliyokuwa imefungwa na Idara ya Ukaguzi ya wilaya baada ya wanafunzi wake kujisaidia vichakani kwa kukosa huduma hiyo.
 
Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Patrck Karangwa amewaambia Madiwani katika Baraza lao la kawaida kuwa alishtushwa na taarifa ya kufungwa shule hiyo kupitia vyombo vya habari.
 
Amesema juzi katuma wataalamu kwenda eneo la Bugarama lililo kwenye Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu kwa ajili ya kwenda kujenga vyoo hivyo ambavyo vimesababisha shule hiyo kufungwa.
 
Hata hivyo amesema Mgodi huo wa Bulyanhulu kwa kushirikiana na wananchi wamechanga kiasi cha shilingi Milioni Nane kwa ajili ya ujenzi wa vyoo hivyo.
 
Mwanzoni mwa juma hili Idara ya ukaguzi wa shule za Msingi wilaya ya Kahama,iliifunga shule hiyo baada ya kubaini wanafunzi zaidi ya 1,500 hawana pa kujisaidia kutokana na shule hiyo kutokuwa na Vyoo.
 

0 comments:

 
Supported by Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Shinyanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa