Na Magdalena Nkulu- Shinyanga
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe.Ally N.Rufunga amezindua rasmi bodi ya Hospitali ya Rufaa ya mkoa katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa mkoa mapema leo.
Bodi hiyo imezinduliwa kufuatia mkakati wa Wizara ya afya na Ustawi wa jamii wa kuimarisha uwezo wa hospitali za mikoa na kanda kuweza kutoa huduma bora kwa kuwa na bodi zenye uwakilishi wa jamii.
Akizindua bodi hiyo ambayo ni ya kwanza katika historia ya Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga,Mhe.Rufunga amesema chombo hicho ni cha uwakilishi wa wananchi hivyo amewataka wajumbe wa bodi hiyo kujenga ushirikiano na uhusiano na wadau wa huduma za afya ili kuleta mabadiliko katika sekta ya afya.
Aidha, Rufunga ametoa rai kwa wajumbe wa bodi kufanya vikao kwa mujibu wa sheria na taratibu na hasa kutekeleza maazimio ya vikao kwani wajibu walionao ni kwa ajili ya maisha ya watu hivyo wasifanye kazi kwa mazoea bila kutekeleza maazimio.
Amesema iwapo bodi hiyo itasimamia vema huduma zitolewazo na hospitali ya rufaa ya mkoa, ikiwamo vyanzo vya mapato na matumizi,upatikanaji wa miundombinu,madawa na vifaa tiba,viwango vya huduma vitakuwa bora zaidi na hivyo kuimarisha afya za wananchi wa mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe.Ally N.Rufunga akitoa hotuba ya ufzinduzi wa Bodi ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga leo katika ukumbi wa mikutano ofisini kwake
Baadhi ya wajumbe wa bodi ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wakimsikiliza Mhe.Mkuu wa Mkoa Ally N. Rufunga akizindua bodi ya Hospitali ya mkoa.
Picha ya pamoja,Mhe.Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Ally N. Rufunga pamoja na wajumbe wa bodi ya Hospitali ya Rufaa ya mkoa iliyozinduliwa leo katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa Shinyanga.(Picha zote na Magdalena Nkulu - Ofisi ya mkuu wa mkoa Shinyanga)

0 comments:
Post a Comment