SHULE ya Msingi Bugarama ambayo ipo katika eneo linalozunguka Mgodi
wa dhahabu wa Bulyanhulu unaomilikiwa na Kampuni ya African Barrick
Gold Mines Ltd imefungwa baada ya kukosa vyoo.
Mkaguzi Mkuu wa Shule za Msingi wilayani Kahama, Ephraim Kaijuko,
alisema jana kuwa shule hiyo ilifunguwa juzi baada ya kubaini wanafunzi
1,500 wanaosoma hapo hawana pa kujisaidia na badala yake hujisaidia
vichakani.
Alisema idara yake sasa inazunguka wilaya nzima kufanya ukaguzi wa
mapungufu mbalimbali yaliyomo kwenye shule za msingi huku kubwa zaidi
likiwa ni vyoo.
Wilayani Kahama idadi kubwa ya shule za msingi hazina vyoo baada ya
vilivyokuwepo kupitia mpango wa MMEM kubomoka na vingine kuchakaa baada
ya kujengwa chini ya kiwango.
Aidha, katika mpango huo wa MMEM hakukuwa na jitihada nyingine za
ujenzi wa vyoo vingine licha ya idadi ya wanafunzi kuongezeka kila
mwaka na kufanya vilivyokuwepo kuzidiwa matumizi.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment