Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MWANAFUNZI wa darasa la tatu katika Shule ya Msingi Majengo
wilayani Kahama, Shinyanga, Said Siraji (13), amenusurika kufa baada ya
kuchinjwa shingo na baba yake mzazi.
Hivi sasa mtoto huyo amelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kahama
ambapo Mganga Mkuu wa hospitali hiyo Dk. Joseph Fwoma alikiri kumpokea
mwanafunzi huyo jana alfajiri baada ya kuokolewa na raia wema wakati
akikimbia huku akivuja damu shingoni.
Dk. Fwoma alisema alipofika hospitalini hapo madaktari walimfanyia
upasuaji na kumshona sehemu ya koromeo lililochinjwa huku akibainisha
kwamba hali yake inaendelea vizuri baada ya kuongezwa damu.
Chanzo;Tanznia Daima
0 comments:
Post a Comment