Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Wengi tumekuwana tukizifahamu aina mbalimbali za njugu kama vile karanga,korosho na nazi.
Lozi ni moja wapo ya njugu ambazo jina lake
maarufu duniani ni Almonds. Yenyewe hukaangwa kidogo na huliwa kwa
kutafunwa kama ilivyo karanga.
Kitafunwa hiki kinachofanana na karanga kinatajwa
kuwa ni tiba kwa watu wenye matatizo ya moyo na husaidia kwa kiasi
kikubwa katika kuratibu mapigo ya moyo.
Pamoja na hilo utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu
cha Purdue unaonyesha lozi kuwa na manufaa mengi kiafya ukilinganisha na
aina nyingine za njugu.
Hiyo inatokana na kiwango kikubwa cha protini na
virutubisho vingine kama vile madini na kusaidia kuratibu mfumo mzima wa
mwili, moja wapo maradhi ya moyo.
Mtafiti katika Bodi ya Sayansi Jimbo la California
nchini Marekani, Dk Karen Lapsley ambaye ni mmoja wa wataalam
walioshiriki katika utafiti huo anasema lozi pia inasadia kwa kiasi
kikubwa kupunguza kasi ya ugonjwa wa kisukari.
Anasema kuwa mtu mwenye kisukari anapotafuna lozi
zinamsaidia kuratibu mfumo wake damu na kuhakikisha siku zote mishipa ya
damu inakuwa inafanya kazi inavyostahili.
Dk Penny Kris Etherton wa chuo kikuu cha
Pennsylvania anasema lozi zina uwezo mkubwa wa kupunguza kiwango cha
lehemu ndani ya mwili.
Madini yaliyomo kwenye lozi yanasaidia kuimarisha
mifupa, misuli, viungo na kukabiliana na shinikizo la damu. Matatizo
haya mara nyingi hujitokeza kjwa wenye umri mkubwa.
Chanzo:Mwananchi
Chanzo:Mwananchi
0 comments:
Post a Comment