Home »
» TAMASHA LA PASAKA LAKONGA NYOYO ZA MASHABIKI MJINI SHINYANGA
TAMASHA LA PASAKA LAKONGA NYOYO ZA MASHABIKI MJINI SHINYANGA
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mwimbaji
wa muziki wa injili Rose Muhando akiimba kwenye uwanja wa Kambarage
mjini Shinyanga wakati wa Tamasha la Pasaka lililofanyika mkoani humo
likishirikisha waimbaji mbalimbali wa muziki wa injili, Tamasha hilo
limeandaliwa na kampuni ya Msama Promotion na linaendelea Kesho kwenye
uwanja wa CCM Kirumba ambapo Mwanamuziki maarufu wa muziki wa injili
kutoka nchini Afrika Kusini Rebecca Malope atafanya mambo mamkubwa
jijini Mwanza.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-SHINYANGA)
Kundi la wanenguaji wa mwimbaji Rose Muhando wakifanya vitu vyao kwenye uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga leo.
Mwimbaji Rose Muhando akicheza na watoto wakati alipokuwa akiimba katika Tamasha la Pasaka mjini Shinyanga leo.
Mwimbaji
wa muziki wa injili Upendo Kilahiro akiimba jukwaani huku akipigwa tafu
na waimbaji wenzake wa muziki wa injili kutoka kushoto ni Grace
Mwikwabe, Tumaini Njole, Faraja Ntaboba kuoka nchini Congo DRC na Mess
Chengula.
Mwimbaji
Upendo Nkone wa pili kutoka kulia akicheza na waimbaji Faraja Ntaboba
kulia na wenzake Grace Mwikwabe kushoto na Tumaini njole wakati
alipokuwa akifanya vitu vyake jukwaani
Faraja
Ntaboba mwimbaji wa muziki wa injili kutoka Congo DRC akifanya vitu
vyake mbele ya mashabiki kwenye uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
Faraja
Ntaboba mwimbaji wa muziki wa injili kutoka Congo DRC akifanya vitu
vyake mbele ya mashabiki kwenye uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
Mwimbaji Mess Chengula naye alifanya mambo makubwa katika tamasha hilo.
Mess Chengula akionyesha uwezo wa ktawala jukwaa katika tamasha hilo.
Mwimbaji
Grace Mwikwabe akifanya vitu vyake ambapo kesho anatarajiwa kuzindua
albam yake kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Mwimbaji Tumaini Njole amefanya mambo makubwa pia.
Mashabiki
wa muziki wa injili waliohudhuria katika tamasha hilo wakipata burudani
kutoka kwa waimbaji mbalimbali katika tamasha hilo.
Hapa ni Fullburudani
0 comments:
Post a Comment