Home » » UKAWA WASUASUA KWENDA MAHAKAMANI

UKAWA WASUASUA KWENDA MAHAKAMANI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Freeman Mbowe
 
Vyama  vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), wameshindwa kutimiza kusudio lao la kwenda kufungua kesi Mahakama Kuu kuhoji mamlaka ya Bunge Maalumu la Katiba.
Jumatatu iliyopita Wakili wa Chama Cha Wananchi (CUF), Twaha Taslima, alinukuliwa na gazeti moja la kila siku akisema kwamba wanatarajia kwenda mahakamani kufungua kesi hiyo.

Hata hivyo, kwa siku mbili mfululizo Jumanne na Jumatano hakuna wakili yeyote wa UKAWA aliyefika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kufungua kesi hiyo dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

Walipopigiwa simu kwa nyakati tofauti mawakili hao ambao hawakutaka majina yao yatajwe, walisema kwamba tayari wameshaandaa hati kwa ajili ya kufungua kesi hiyo na kwamba wakati wowote kesi hiyo itafunguliwa.
SOURCE: NIPASHE

0 comments:

 
Supported by Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Shinyanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa