Home » » BARRICK WAGAWA MICHE SHINYANGA

BARRICK WAGAWA MICHE SHINYANGA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

KAMPUNI ya uchimbaji wa madini ya dhahabu ya African Barrick Gold Mine wilayani Kahama, Shinyanga, imegawa miche ya miti ya matunda 3,000 kwa wakazi wa Kijiji cha Ishilabela, Kata ya Pandagichiza, Wilaya ya Shinyanga Vijijini kwa lengo la kutunza uoto wa asili.
Wakizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Mazingira duniani juzi, Ofisa Mazingira wa kampuni hiyo, Naziri Eliakimu, alisema msaada huo unaonyesha namna wanavyoshirikiana na jamii kutunza mazingira.
Alisema Barrick imekuwa ikitoa elimu ya kupanda miti na kuitunza, ndiyo maana wameamua kuotesha miche mbalimbali ya miti kati ya 30,000 hadi 50,000 kila mwaka na kuigawa kwa wananchi bila malipo.
Eliakimu alisema kampuni hiyo imekuwa makini na utunzaji wa mazingira kuhakikisha maji yenye kemikali hayatoki nje ya kampuni na kuathiri wananchi.
‘Migodi mingi hapa nchini inalalamikiwa kutiririsha maji yenye kemikali kwa wananchi na kuleta athari mbalimbali.
“Hivyo, tumeanza utaratibu wa kuchimba mabwawa ya kutunzia maji hayo ambayo chini yake yana plastiki ambazo hazipitishi maji, hivyo kuishia humo humo ndani ya kampuni na kuyafanyia utaratibu wa kitaalamu.
“Kemikali hizi zinapopita chini ya ardhi na kuingia katika mazingira yanayotumiwa na watu huleta madhara makubwa ikiwemo kuathiri uzalishaji wa mazao,” alisema.
Chanzo;Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Shinyanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa