Home » » VIFOVYA WAJAWAZITO VYAONGEZEKA SHINYANGA

VIFOVYA WAJAWAZITO VYAONGEZEKA SHINYANGA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
VIFO vya wajawazito vimeongezeka mkoani hapa kutokana na ukosefu wa hospitali za wilaya na vituo vya afya vya kutosha, huku wengi wakilazimika kujifungulia njiani wakifuata huduma za uzazi.
Akizungumza katika warsha ya siku moja ya kujadili mikakati ya kupunguza vifo vya mama na mtoto, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Ntuli Kapologwe, alisema mwaka 2012 vifo vya wajawazito vilikuwa 46, lakini mwaka jana viliongezeka hadi 61 kati ya wajawazito 100,000 waliojifungua kipindi hicho.
Kapologwe alisema Shinyanga ina hospitali moja tu ya wilaya iliyoko Kahama, huku vituo vya afya vilivyopo katika wilaya nyingine vikiwa vichache na visivyokidhi huduma ya afya na visivyokuwa na miundombinu bora ya afya.
Alisema vituo vyote havina umeme, na hivyo kufanya wajawazito kujifungulia gizani. Kwamba havina majengo ya kutosha, upungufu wa wauguzi, vitendea kazi na ukosefu wa upatikanaji wa damu salama na ya kutosha pale mzazi anapohitaji kuongezewa.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Ally Rufunga, alisema mkakati wa kupunguza vifo vya mama na mtoto ni agizo la Rais Jakaya Kikwete aliyeagiza kila mkoa upunguze vifo hivyo ndani ya miaka miwili.
Aliagiza elimu itolewe kwa jamii kujua umuhimu wa kuchangia Mfuko wa Bima ya Afya (CHF) ambao utasaidia kupatikana kwa dawa nyingi za matibabu.
Chanzo:Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Shinyanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa