Home » » UKAWA WAMALIZA ZIARA MIKOANI

UKAWA WAMALIZA ZIARA MIKOANI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willbrod Slaa
 
Vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vimehitimisha ziara yake ya siku 14 baada ya kutembelea mikoa 17 huku vikitangaza kugawana majukumu ya namna vitakavyopambana na Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mkuu wa 2015.
Vyama hivyo vya Chadema, NCCR-Mageuzi na CUF, viongozi wake wandamazi nje ya Bunge walianza ziara ya kutembelea mikoani kuwaelimisha wananchi umuhimu wa katiba

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya NCC-Mageuzi, Hemed Msabaha, akizunguma katika mkutano wa hadhara w uliofanyika mjini Geita, juzi alisema umoja wao umejipanga kupambana na CCM katika uchaguzi mkuu wa 2015.

Msabaha alisema wamepeana majukumu ambayo Chadema kitakuwa kinafanya mashambulizi ya angani kwa kufanya ziara
mikoani kwa kutumia helkopita  nchi nzima.

Alisema CUF kinachoongozwa na Mwenyekiti wake,Profesa Ibrahimu Lipumba, kimepewa jukumu la kufanya mashambulizi ya
nchi kavu  ili kuhakikisha CCM haifanyi hila zozote za kuhujumu uchaguzi huo.

Msabaha alisema NCCR-Mageuzi kinaongozwa na James Mbatia, kitaendesha mashambulizi majini lengo likiwa ni kuhakikisha kura haziibiwi mwakani.

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willbrod Slaa, aliwataka wananchi kuwaunga mkono katika harakati za kupata katiba bora na
kupinga hujuma alizodai zinataka kufanywa na CCM kuhujumu katiba mpya.

Dk. Slaa alisema umoja wao utaendelea hadi u2015 na kusisitiza kuwa kama CCM itang’ang’ania suala la muundo wa serikali tatu lisijadiliwe katika Bunge Maalum la Katiba, wabunge wa Ukawa hawatakuwa tayari kurejea katika bunge hilo.
 
SOURCE: NIPASHE

0 comments:

 
Supported by Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Shinyanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa