Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
SHIRIKISHO la Vyama vya
Watu Wenye Ulemavu Wilayani Kahama, mkoani Shinyanga
(SHIVYAWATA)wamezitaka taasisi za fedha zinazotoa mikopo ya ujasiriamali
kuwakopesha baadhi ya wanaohitaji kuchukua mkopo badala ya kuwaona kama
hawawezi na kuwabagua.
Wakizungumza juzi
katika mkutano wa tathmini na ufuatiliaji kuhusu utekelezaji wa sheria
ya watu wenye ulemavu namba 9 ya mwaka 2010 uliofanyika ofisini kwao
mjini Kahama wamezitaka taasisi za fedha zinazotoa mikopo ya
ujasiriamali kuwakopesha kama watu wengine bila ubaguzi.
Bi.Kuruthumu Jafari
alisema baadhi ya watu wenye ulemavu wamekuwa wakijishughulisha na
ujasiriamali mbalimbali, lakini tatizo kubwa wamekuwa wakihitaji msaada
wa kuwezeshwa kukopeshwa waweze kuwa na ufanisi wa kazi yao.
Mwenyekiti wa
SHIVYAWATA wa wilaya ya Kahama, Bw.Marco Kanjiwa alisema watu wenye
ulemavu ni sawasawa na mtu yeyote katika kazi za ujasiriamali na
kuzitaka taasisi za fedha zinazotoa mkopo ziweze kuwakopesha
wanapohitaji.
Akizungumzia kuhusu
sheria namba 9 ya mwaka 2010 inayohusu watu wenye ulemavu iliyotungwa na
bunge Kanjiwa alisema jamii bado haijawa na uelewa kuhusu sheria hiyo
na kuwataka maofisa maendeleo ya jamii kuwaelimisha wananchi na
kuisimamia popote kazini kwao.
Makamu Mwenyekiti wa
SHIVYAWATA wa wilaya ya Kahama Bw.Sitta Masenya alizitaka mamlaka zote
za serikali kuendelea kutoa elimu kwa jamii juu ya sheria ya watu wenye
ulemavu kwa sababu bado miongoni mwa baadhi ya jamii kuna tatizo la
kuwaficha huku wengine wakiendelea kuwabagua na kuwanyanyapa
Chanzo:Majira
0 comments:
Post a Comment