Home » » AFYA: SUMU HUATHIRI WAUME, WATOTO WA WANAWAKE WANAOTUMIA MIKOROGO

AFYA: SUMU HUATHIRI WAUME, WATOTO WA WANAWAKE WANAOTUMIA MIKOROGO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
“Tunafanya kampeni ya kupambana na vipodozi vyenye sumu kwa sababu tatizo ni kubwa nchini.“Hadi sasa asilimia 52 ya Watanzania hutumia mkorogo. matokeo yake wengi wameathirika na wanashindwa kuacha.”

amekuwa akijishughulisha na biashara za vipodozi vya asili, maarufu kama mkorogo.
Hata hivyo, biashara hiyo aliisitisha mwaka 2013 baada ya kupata madhara makubwa ya ngozi ambayo yaliambukiza pia familia yake.
“Nilianza kuwashwa ngozi mfululizo, nikadhani nimeathirika na Ukimwi,” anasema akikumbuka jinsi ugonjwa huo ulivyomtesa.
 “Niliamua kwenda Hospitali ya Muhimbili kwa daktari wa ngozi ambaye alichukua kipande cha ngozi yangu na kwenda kuipima na kubaini tatizo ni mkorogo.”
Nuru anasema alipewa dawa aina ya scaboma ambayo ilimsaidia na inaendelea kumsaidia hadi sasa. Kwa sasa ameachana na biashara hiyo na badala yake anatoa ushuhuda wa madhara ya dawa hizi.
Akizungumzia biashara hiyo, Nuru anasema licha ya kusitisha biashara iliyokuwa ikimpa fedha za kujikimu kimaisha, sasa amekuwa balozi wa kueleza madhara ya mkorogo kwa jamii.
Alianza biashara hiyo mwaka 1998 baada ya kufanya majaribio ya kupaka losheni hizo na kuona zinampendeza na watu wanazipenda na hivyo akawa anachanganya na kuuza.
“Kwa kipimo kimoja nilikuwa nauza kati ya Sh25,000 hadi 30,000 na ningeweza kupata hadi Sh400,000 kwa mwezi,” anasema.
Hata hivyo, mwaka 2013, mambo yalianza kwenda vibaya baada ya kujikuta akiwashwa ngozi na kuharibika ikawa kavu, yenye mikunjo na kubadilika rangi.
Licha ya Serikali kupambana na utengenezaji na matumizi ya vipodozi vyenye sumu, imeelezwa kuwa zaidi ya nusu ya Watanzania hutumia vipodozi hivyo kwa lengo la kuongeza urembo.
Utafiti uliofanywa na Taasisi ya Evirocare ya Dar es Salaam mwaka 2013 umeonyesha bado tatizo hilo ni kubwa.
Utafiti huo ulifanyika kwa kuhusisha mkoa mmoja katika kanda sita nchini. Mikoa hiyo ni Dar es Salaam ukiwakilisha Kanda ya Mashariki, Mbeya (Kanda ya Nyanda za Juu Kusini), Tanga (Kanda ya Kaskazini) na Dodoma (Kanda ya Kati).
“Watoto wanaoathirika zaidi ni wale wanaonyonyeshwa na wanawake wanaotumia mkorogo.”
Wengi hawajui madhara yake
Walipoulizwa kuhusu aina ya kemikali zilizomo kwenye vipodozi wanavyotumia, asilimia 62.4 ya watu 263 walisema hawajui huku asilimia 34 wakisema wanajua.
Unasema pia nusu ya wauzaji walisema hawajui kemikali zitumiwazo katika vipodozi wanavyouza, achilia mbali madhara yatokanayo na vipodozi, hivyo kipaumbele chao ni kupata faida  kuliko afya za watumiaji.
Akizungumzia utafiti huo, meneja mradi wa kupambana na vipodozi vyenye sumu, Euphrasia Shayo anasema hali ni mbaya kwa Tanzania ndiyo maana Envirocare wameanzisha kampeni ya kupambana na vipodozi hivyo.
“Tunafanya kampeni ya kupambana na vipodozi vyenye sumu kwa sababu tatizo ni kubwa nchini. Hadi sasa asilimia 52 ya Watanzania hutumia kati ya Sh35,000 hadi 50,000 kwa mwezi kununua mkorogo. matokeo yake wengi wameathirika na wanashindwa kuacha,” anasema Euphrasia na kuongeza:
“Kichocheo kikubwa ni wanaume ambao huwashawishi wanawake watumie ili wawapende. Tunatoa elimu kwa wanawake kujiamini na uzuri walionao na kutumia vipodozi visivyo na sumu.”
Madhara ya vipodozi
Akizungumzia madhara ya vipodozi hivyo, Shayo anasema kwa kiasi kikubwa cha mikorogo husababisha saratani ya ngozi na kupunguza nguvu za kiume.
Madhara haya pia huwaathiri wale ambao wenzi wao wanatumia vipodozi vyenye viambata vya sumu.
 “Kwa mtu aliyeathirika na matumizi ya mkorogo inabidi atumie dawa kwa miaka mitatu mfululizo huku akipewa ushauri wa kitaalamu.
Siyo rahisi kuacha kwani kwa siku mtu hutumia hadi dawa tisa, hivyo itabidi kuacha moja baada ya nyingine, vinginevyo ataharibika kabisa mwili wake,” anasema.
 Chanzo:Mwananchi

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Shinyanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa