Home » » MIRADI YA ZAIDI YA BIL.10 KUPITIWA NA MWENGE WA UHURU MKOANI SHINYANGA

MIRADI YA ZAIDI YA BIL.10 KUPITIWA NA MWENGE WA UHURU MKOANI SHINYANGA

Mkoa wa Shinyanga utapokea Mwenge wa Uhuru kutoka Mkoa wa Geita tarehe 01 Oktoba 2014 katika kijiji cha Mwabomba,Kata ya Idahina, Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu Wilayani Kahama na utakimbizwa kwa siku sita kabla
ya kukabidhiwa Mkoani Tabora Tarehe 07/10/2014 katika kijiji cha Nata Wilaya ya Nzega.
Mwaka huu 2014 Mwenge wa Uhuru katika Mkoa wa Shinyanga utapitia jumla ya miradi 58, ambapo miradi 5 itazinduliwa, 20 itafunguliwa, 13 itawekewa mawe ya msingi na miradi20 itaonwa. Miradi yote ina thamani
ya Sh. 10,378,951,014. Gharama za miradi yote hii imetokana na nguvu za wananchi, Halmashauri, Serikali Kuu na Wahisani mbalimbali.
Ratiba ya Mwenge wa Uhuru mwaka huu mkoani Shinyanga itakua kama ifuatavyo:
Tarehe 01/10/2014 – Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
Tarehe 02/10/2014 – Halmashauri ya Mji Kahama
Tarehe 03/10/2014 –Halmashauri ya Wilaya ya Msalala
Tarehe 04/10/2014 – Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
Tarehe 05/10/2014 – Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga na
Tarehe 06/10/2014 – Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
Mwenge wa Uhuru hukimbizwa kila mwaka katika Halmashauri zote nchini kuanzia mwezi Mei hadi Oktoba kuhamasisha wananchi, mashirika, taasisi na wadau mbalimbali kuunganisha nguvu zao kuchangia kwa hali na mali kufanikisha miradi miradi ya maendeleo waliyobuni wenyewe katika maeneo yao kulingana na fursa zilizopo na mahitaji yao halisi.
Hivyo, Wananchi wote wa Mkoa wa Shinyanga wanahimizwa kujitokeza katika maeneo yote Mwenge utakapopita ili kushuhudia utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo walizoibua wenyewe.
Ujumbe wa Mwenge Mwaka huu ni ‘Katiba ni Sheria Kuu ya nchi, Jitokeze kupiga kura ya maoni tupate katiba mpya’.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Shinyanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa