Mkuu wa Mkoa akizungumza na wananchi waliohudhuria maadhimisho hayo kijijini Lunguya
Baadhi ya wananchi na wadau mbalimbali wakifuatilia kwa makini burudani zilizokuwa zikiendelea katika maadhimisho ya siku ya UKIMWI yaliyofanyika jana kimkoa wilayani Kahama mkoani Shinyanga
Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Ally N. Rufunga akielekea kukagua mabanda ya wadau wa UKIMWI katika kijiji cha Lunguya wilaya ya Kahama ambako maadhimisho ya siku ya UKIMWI yalifanyika kimkoa,akiwa ameambatana na Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Ntuli Kapologwe
Mkuu
wa Mkoa wa Shinyanga Ally N. Rufunga akikagua na kupata maelezo kwenye
baadhi ya mabanda ya wadau wanaoshirikiana na serikali katika kusaidia
kupunguza maambukizi ya VVU mkoani Shinyanga
Walemavu wa viungo wakitoa burudani mbele ya Mgeni rasmi Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga katika maadhimisho hayo
Wasichana
wanaosaidiwa na shirika la Kiwohede wakitoa burudani mbele ya mgeni
rasmi Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga katika maadhimisho hayo
Watoto wa shule ya Msingi Lunguya wakionesha vipaji vyao katika bunge la watoto kwenye maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani
Wananchi wa wilaya ya Kahama waliodhuria sherehe hizo wakimsikiliza Mhe. Mkuu wa Mkoa
Mkuu wa Mkoa wa
Shinyanga Mhe. Ally N. Rufunga amewaasa wananchi kuitumia siku ya UKIMWI
duniani kuwa siku ya kuwakumbuka watu wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi na
kutafakari juu ya mbinu bora za kuwahudumia na kuwaondolea unyanyapaa
pamoja na kuwakumbuka yatima ambao wamefiwa na wazazi kutokana na
maradhi yanayohusiana na UKIMWI.
Mhe.
Rufunga amesema hayo jana, katika maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani
yaliyofanyika kimkoa wilayani Kahama katika Halmashauri ya Msalala
kijiji cha Lunguya.
Rufunga
amesema hali ya ugonjwa wa UKIMWI mkoani hapa bado ni mbaya kwani
ushamiri wa maambukizi uko juu ya kiwango cha Taifa cha asilimia 5.1
kutokana na tafiti za kisayansi za mwaka 2011 hadi 2012, kwa mujibu wa
tafiti hizo mkoa wa Shinyanga una ushamiri wa maambukizi asilimia 7.4.
Aidha,
takwimu za ndani ya mkoa zilizotokana na huduma zote za upimaji wa VVU
kwa kipindi cha Januari hadi Oktoba, mwaka huu 2014, zinaonesha
ushamiri wa maambukizi ni asilimia 5.01 sawa na pungufu ya asilimia 0.89
kutoka 5.9 ya mwaka 2013 hivyo ametoa rai kwa wananchi wote kupima na
iwapo watagundulika wana maambukizi watembelee vituo vya afya ili
kuendelea kupata huduma za matunzo na tiba.
Hadi
kufikia mwezi Oktoba 2014 Mkoa umesajili zaidi ya watu elfu 58
wanaoishi na virusi vya UKIMWI na kati yao watu 22,231 wanaendelea
kutumia dawa za kufubaza virusi vya UKIMWI.
Na Magdalena Nkulu
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Shinyanga
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment