MKOA wa Shinyanga umeelezwa kuongoza kwa vitendo vya kikatili kama vile ubakaji, ndoa za utotoni, imani za kishirikina na kuitaka jamii kubadilika ili kuweza kutokomeza vitendo hivyo.
Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa dawati la Jinsia taifa, Naibu Kamishna wa Polisi, Adolphine Kyalo katika kilele cha maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili na siku ya haki za binadamu iliyoadhimishwa katika viwanja vya Shy-com mjini Shinyanga.
Kyalo alisema kuwa wananchi wa mkoa wa Shinyanga wanatakiwa kubadilika kwa kushirikiana na polisi ili kuweza kutokomeza vitendo vya kikatili kwa wanawake pamoja na kuondokana na mimba za utotoni.
Amesema mkoa wa Shinyanga unaongoza kitaifa katika masuala ya ukatili kwa asilimia 59 .
Chanzo:Habari Leo
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment