Home » » HATARI..KICHANGA CHA MWAKA MMOJA CHAKUTWA KIMETUPWA JALALANI HUKO WILAYANI KAHAMA MKOANI SHINYANGA

HATARI..KICHANGA CHA MWAKA MMOJA CHAKUTWA KIMETUPWA JALALANI HUKO WILAYANI KAHAMA MKOANI SHINYANGA



Wananchi wa mtaa wa nyahanga mjini Kahama wakiangalia mwili wa kichanga hicho kilichowekwa kwenye mfuko.
Mwili wa mtoto mwenye umri wa siku 1 umekotwa ukiwa umetupwa katika eneo la dampo la shule ya msingi Nyahanga wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Mashuhuda watukio hilo wamesema kuwa mwili wa mtoto huyo umegunduliwa jana na wanafunzi wa shule ya msingi Nyahanga wakati wanaenda kutupa takataka kwenye dampo hilo.
Akizungumzia tukio hilo afisa mtendaji wa kata ya Nyahanga Nambo Ntaki amesema kuwa wananchi wa mtaa huo wanapaswa kutoa ushirikiano ili kuweza kumbaini mtu ambaye ametekeleza tukio hilo ambalo ni la kinyama.


Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa huo Wiliam Upamba amesema kuwa wananchi wanapaswa kukomesha matukio kama hayo ambayo yanaleta sifa mbaya kwenye jamii.


Mwili wa mtoto huyo umekabidhiwa kwa viongozi wa mtaa wa nyahanga na jeshi la polisi kwaajili ya taratibu za mazishi na kutoa wito kwa wananchi kushirikiana jeshi la polisi kwa lengo la kumbaini mtu ambaye ametekeza tukio hilo.
Chanzo Vijimambo Blog

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Shinyanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa