Naibu
Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga (aliyesimama) akitoa
hotuba yake mwanzoni mwa ziara yake ya kutembelea mgodi wa dhahabu wa
Bulyanhulu ulioko wilaya ya Msalala, mkoani Shinyanga, Jumamosi Aprili
11, 2015. Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya uchimbaji madini
ya Acacia, Brad Gordon, na kulia ni makamu wa rais wa kampuni hiyo
anayeshughulikia masuala ya kampuni hapa Tanzania, Deo Mwanyika.
Kaimu
Meneja Mkuu mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu ulioko wilaya ya Msalala,
mkoani Shinyanga, Benedict Busunzu, akizungumza shughuli za uchimbaji
madini za mgodi huo na huduma zitolewazo kwa jamii, wakati naibu waziri
wa jishati na madini, Charles Kitwanga, alipofanya ziara ya kutembelea
mgodi huo, Jumamosi Aprili 11, 2015.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa kampuni ya uchimbaji madini ya Acacia, Brad Gordon,
akizungumza wakati wa uwasilishaji shughuli mbalimbali zifanywazo na
migodi inayomilikiwa na kampuni hiyo hapa nchini ya Bulyanhulu, North
Mara na Buzwagi, wakati wa ziara ya naibu waziri wa nishati na madini,
Charles Kitwanga, alipotembelea mgodi wa Bulyanhulu uliko wilaya ya
Msalala mkoani Shinyanga, Jumamosi Aprili 11, 2015.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa kampuni ya uchimbaji madini ya Acacia, Brad Gordon,
(wapili kushoto), akimpa maelezo Naibu Waziri wa Nishati na Madini,
Charles Kitwanga, (watatu kushoto), alipotembelea eneo la chini ya ardhi
la mgodiwa Bulyanhulu kiasi cha kilomita 1.5 chini ya bardhi, Jumamosi
Aprili 11, 2015. Kushoto ni mwenyekiti wa kampiuni ya uchimbaji dhahabu
ya Mlalo, Mohammed Hussein.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa kampuni ya uchimbaji madini ya Acacia, Brad Gordon,
(Kulia), akikabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni 749.53, Afisa
Mipango wa Halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shjinyanga, Mophen
Mwakajonga, ikiwa ni kodi ya huduma (service levy), huku Naibu Waziri wa
Nishati na Madini, Charles Kitwanga (katikati) akishuhudia. Hafla hiyo
ilifanyika kwenye mgodi wa Bulyanhulu ulioko wilayani humo April 11,
2015.
Sehemu
ya Ujumbe ulioambatana na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles
Kitwanga katika ziara ya mgodi wa Bulyanhulu April 11, 2015.
Naibu
waziri wa nishati na madini, Charles Kitwanga, (wakwanza kushoto) na
ujumbe wake, wakipatiwa maelezo ya kiusalama muda mfupi kabla ya kuanza
ziara ya kutembelea shughuli za uchimbaji madini chini ya ardhi kwenye
mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu uliko wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga
Jumamosi Aprili 11, 2015.
Naibu
waziri wa nishati na madini, Charles Kitwanga, (kushoto), na Afisa
Mtendaji Mkuu wa kampuni ya uchimbaji madini ya Acacia, Brad Gordon,
(kulia), wakimsikiliza mtaalam wa shughuli za uchimbaji madini ardhini,
wa mgodi huo, wakati wa ziara ya naibu waziri Jumamosi Aprili 11, 2015.
Naibu
Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga (kushoto) akipeana mkono
na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya uchimbaji madini ya Acacia, Brad
Gordon, wakati alipowasili kutembelea mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu,
ulioko wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga, Jumamosi Aprili 11, 2015.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment