Mraghabishi mwalimu Revocatus Renatus ( kulia ) wa kijiji cha Unyanyembe mkoani Shinyanga akihojiwa na mtangazaji wa Redio Free Africa Felista Kujirilwa wakati wa kuandaa moja ya vipindi vya redio vya Chukua Hatua.
“Haijatokea hata
siku moja mwandishi wa habari akaja huku kwa kweli. Hii ni mara yangu ya
kwanza kuona
wanahabari katika kijiji chetu. Toka nimezaliwa sijawahi kumuona mwandishi wa
habari kuja hapa na mimi nina miaka 70.” Hayo ni maneno ya Mzee Titus Ndugulile
mraghabishi wa kijiji cha Mwamala-B kilichopo kata ya Mwamala wilaya ya
Shinyanga vijijini.
Kijiji hicho
kina wakazi wanaokaribia 2,820 toka katika vitingoji vya Mwanundi, Igegu, Witasisa
na Wela. Yeye ni mmoja kati ya waraghabishi 400 waliosambaa katika vijiji zaidi
180 vilivyopo katika mikoa ya Geita, Simiyu, na Shinyanga. Kundi hili la
waraghabishi linawajumuisha wakulima, viongozi wa dini, madiwani, wenyeviti wa
vijiji, walimu, wanafunzi, wanawake viongozi na wafugaji wanaofanya kazi na
programu ya redio ya Chukua Hatua inayorushwa na redio Kahama FM, Faraja FM, na
Radio Free Afrika.
Redio hizi
zimeanza kufanya kazi na Chukua Hatua kuanzia mwezi Novemba 2012 zikiwa na
lengo la kutoa
fursa na nafasi kwa waraghabishi kuwakilisha mawazo, shida na vipaumbele vyao
kwa viongozi ili waweze kusikiliza kero zao na kuzifanyia kazi. Lakini pia
kuongeza wigo wa vyanzo vipya vya habari kwa vyombo hivyo. Waandishi hawa
walitambulishwa
Kwa waraghabishi
kupitia mafunzo, ziara za ufuatiliaji na uwezeshwaji wa wananchi katika
kung’amua
matatizo yao na kupendekeza njia ya kuyatatua. Mafunzo na ziara hizi zilikuwa
zinafanywa mashirika ya ADLG na CABUIPA ambao ni washirika watekelezaji wa
programu ya Chukua Hatua katika maana ya uwezeshaji wananchi. Matukio haya ya mafunzo na ZA `WWW3ziara ndio
njia ya kwanza iliyotumika kuwatambulisha na kuwakutanisha waandishi na
waraghabishi katika vijiji wanavyotoka. “ Huku ni l i k uwa si j awahi kufika ni mara
yangu ya kwanza na kiukweli watu wamefunguka sana kuhusu matatizo yao.
Kila mtu anataka kuongea nasi
mambo ni mengi na watu wanahamu ya kupaza sauti z a o n a wa
n a t a k a k u s i k i k a ,
”anafafanua mtangazaji wa Redio Free Afrika Felista Kujirilwa baada ya
kutembelea kijiji cha Mwambasha mkoani Shinyanga. Waraghabishi hawa
wamepatiwamafunzo yaliyowawezesha kutambua haki na majukumu yao katika kuleta
mabadiliko ya kweli katika jamii zao. Wameweza pia kuchukua hatua mbalimbali
kwa kushirikiana na wanajamii wengine katika
maeneo wanayotoka ila walikuwa wanakosa sehemu
ambayo wangeweza kupaza sauti zao zaidi tukiacha
mikutano ya vijiji na
kwenye midahalo
wanayoiandaa. Hivyo redio hizi zimeweza kutoa
nafasi kwa waraghabishi nasauti zao
zinasikika na viongozi wao wanasikia na kuchukua hatua stahiki. Kama anavyoelezea
mtangazaji wa Kahama
FM William Bundala ambaye pia anajulikana kama Kijukuu na wasikilizaji wake. “Baada
ya kutoa taarifa za nyumba kupata nyufa kubwa kutokana na milipuko ya baruti
inayolipuliwa kwenye mgodi wa Buzwagi unaomilikiwa na kampuni ya Barrick, mkuu wa
wilaya ya Kahama ameunda kamati maalumu ya kufuatilia suala hilo ili kuweza
kulitolea maamuzi. Tunaendelea kufuatilia kujua nini kitatokea, kubwa ikiwa ni
kulipwa fidia kwa wale ambao nyumba zao zimeharibika.”
Lengo mojawapo
la program ya redio ya Chukua Hatua ni kuhakikisha kwamba viongozi na wenye
dhamana wanachukua hatua kwa kusikiliza matakwa ya wananchi. “Tunawashukuru
sana waandishi wa Kahama FM na hasa Kijukuu kwa kazi nzuri wanayoifanya. Kama
wasingekuja hapa sidhani hata kama mkuu wa wilaya angeweza kumtuma mwakilishi
wake kuja zungumza nasi. Tutaendelea kuitumia redio hii mpaka pale haki itapotendeka
kwa viongozi wetu,” anaelezea Halid Abdu mkazi wa kijiji cha Shenda wilaya ya Gombwe mkoani Geita. Hii ilikuwa baada ya redio Kahama FM kurusha
matangazo ya moja kwa moja ya mkutano wa kijiji ulioamua kuwatoa viongozi wa
kijiji kwa tuhuma za kutumia vibaya fedha zinazotokana na vitega uchumi vya
kijiji; ikiwamo makrasha, wachimbaji wadogo wadogo na malori yanayobeba mchanga
katika mgodi mdogo unaomilikiwa na kiijiji hicho cha Shenda. Baada ya habari hiyo
kurushwa redioni mkuu wa wilaya alilazimika kumtuma Mkurugenzi wake kwenda
katika kijiji hicho ili kuongea na wananchi kuhusu kilio chao. Makutano haya
baina ya waandishi wa habari na waraghabishi
Haya yamewezesha
redio kupata vipindi mbalimbali nje ya mambo ya
Chukua Hatua. “Hapa pana stori
nyingi tofauti za kufanya, tumeongea na huyu binti, maskini kumbe ameambukizwa virusi
vya ukimwi na ametueleza mambo mengi yanayotokea pale njia panda ya Tinde.
Inabidi tufike hapo ili tufanye kipindi cha TV
kuhusu tatizo la Ukimwi na jinsi mabinti wanavyojiuza,” anaelezea Regina
Mwalekwa wa kituo cha TV cha Clouds alipotembelea kijiji cha Kitule. Si hivyo
tu vipindi vingine vinatumika katika taarifa za habari na hasa mafunzo ya
waraghabishi
hasa ya viongozi
wa dini, lakini pia waandishi wa redio hizi wangeweza kurekodi sauti za wanawake pia kwa ajili ya vipindi vya wanaawake na maendeleo
Lakini pia kuna taarifa ya habari baadhi ya
matukio ambayo waraghabi shi wameweza
kuyaelezea yametumika katika habari na zinasomwa redioni mfano tukio la wananchi
wa kata ya Dutwa kuiomba serikali kupitia wizara ya Ardhi nyumba na maendeleo
ya makazi kutoa semina juu ya sheria za ardhi kwa mabaraza ya ardhi vijijini ili
kupunguza migogoro ya ardhi inayosababisha vifo. Habari hiyo iliyotumika June 6 2013 saa kumi
kamili jioni na saa tatu usiku iliandikwa na mwaandaaji wa vipindi vya Chukua
Hatua wa redio Kahama FM William Bundala. Ambapo mmoja wa wanakijiji hao Masalu
Lugodisha, wa mjini Bariadi amesema, kutokana Jumuia ya Afrika
Mashariki
kuungana, thamani ya ardhi itakuwa kubwa hivyo ni bora serikali ikalijua hilo
mapema na kuanza kuepusha migogoro kwa wananchi. Mpaka jumla ya vipindi 53 vimerushwa na redio
hii vikiwamo vipindi 5 vya TV katika kituo cha Clouds. Huku wasanii wa Chukua Hatua
toka katika wilaya za Maswa, Kahama na Shinyanga vijijini wakijiandaa kuigiza vipindi
vya redio baada ya kumaliza mafunzo yao mwezi wa Juni 2013. Lakini si hilo tu
madiwani wa kata za wilaya ya Bariadi wamenufaika na vipindi hivi kwa kuelezea mambo
waliyoyafanya katika maeneo yao ikiwamo kupata mrejesho toka wa wapiga kura wao
ni kwa kiasi gani wameweza kutimiza ahadi zao na hivyo kujiwekea mazingira mazuri
ya kuchaguliwa tena.
Walimu waraghabishi nao wameweza kuelezea
mikakati na jinsi wanavyofanya kazi na wanajamii katika kujikomboa na ujinga. Mfano
mzuri ni waraghabishi walimu wa wilaya ya Kishapu na hasa kata ya Uchunga. Kwa
sasa programu hii ina waraghabishi zaidi ya 350. Akishangaa jinsi program ya Chukua
Hatua inavyozidi kukua mmoja Wa waraghabishi waanzilishi wa mwaka 2010, Titusi Ndugulile wa
kijiji cha Mwamala B mkoani Shinyanga alisema,
0 comments:
Post a Comment