Idadi
ya wafanyakazi hewa katika mkoa wa Shinyanga ambao awali ulidaiwa
kutokuwa na wafanyakazi hao kabisa, imeongezeka na kufikia 226.
Hayo
yamebainishwa leo na Rais John Magufuli katika uzinduzi wa Daraja la
Kigamboni, ambapo alisisitiza kuwa serikali yake haitawafumbia macho
viongozi ambao kwa namna moja au nyingine wataruhusu mianya ya
ubadhirifu wa fedha katika maeneo yao.
”Mkoa wa Shinyanga kwa taarifa nilizonazo hadi sasa wameshapatikana
wafanyakazi hewa 226 kutoka ‘zero’ hivyo ni lazima tuwajibike kwa
watanzania wanyonge,” amesema Rais Magufuli.
Wakati wa kuwasilisha ripoti ya Mikoa Serikalini aliyekuwa Mkuu wa Mkoa
wa Shinyanga Anne Kilango Malecela alisema mkoa wake hauna mtumishi hewa
hata mmoja jambo lililopelekea Rais Magufuli kuunda tume iliyobaini
watumishi hewa 45 katika awamu ya kwanza.
Baada ya kubainika uwepo wa watumishi hao, Raisi alitangaza kutengua
uteuzi wa Mkuu huyo wa Mkoa kwa kutokuwa makini na taarifa anazopewa na
wasaidizi wake.
0 comments:
Post a Comment