TAARIFA
KWA WADAU WA HABARI MKOA WA SHINYANGA KUHUSU WATU WASIO WAANDISHI WA
HABARI KUTUMIA JINA LA UANDISHI WA HABARI KWA MANUFAA YAO BINAFSI
Klabu
ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club-SPC)
inapenda kuwataarifu wadau wa habari mkoa wa Shinyanga kuwa makini na
baadhi ya watu ambao wamekuwa wakidanganya kuwa ni waandishi wa habari
wakati siyo waandishi wa habari.
Miongoni
mwa watu wanaotumia majina ya vyombo vya habari kutapeli na kujipatia
fedha ni Emmanuel Mpanda ambaye kwa nyakati tofauti amelalamikiwa na
wadau wa habari pamoja na baadhi ya waandishi wa habari kuwa amekuwa
akijiita mwandishi wa habari akitumia majina mbalimbali ya vyombo vya
habari hasa Televisheni na kusababisha usumbufu pale wadau wanapohitaji
kuona habari zao.
Klabu
hii pia inafuatilia mienendo ya watu wengine wawili ambao pindi
uchunguzi wetu utakapokamilika na kubaini udanganyifu wanaoufanya kwa
wadau wa habari kwa kuwahadaa kuwa ni waandishi wa habari nao tutawaweka
hadharani na kuviomba vyombo vya dola kuwachukulia hatua za kisheria.
Tunapenda
kuwatahadharisha kuwa makini na watu wa namna hiyo ambao wanajiita
waandishi wa habari wakati siyo waandishi wa habari kwani mbali na
kuvichafulia majina vyombo vya habari pia wanashusha thamani taaluma ya
Habari,huku wakitutia doa tunaohusika na tasnia hii kwa kuonekana sote
hatufai.
Ili
kuhakikisha kuwa jamii inapata taarifa sahihi na kwa wakati muafaka
tunaomba wadau wote wa habari muendelee kushirikiana na waandishi wa
habari kwani jamii bila habari ni sawa na usiku wa giza.
Tunaomba
wadau wa habari pale panapotokea shughuli ama tatizo lolote msisite
kuwasiliana na ofisi ya Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga
kwa kufika moja kwa moja ofisini au kupitia mawasiliano yaliyopo hapo
juu.
Tunatoa
rai kwa waandishi wa habari kuwa na uchungu na taaluma yao na
kutoruhusu tasnia ya habari kuchezewa kwa kuona haya kuwafichua
Makanjanja ama kwa lugha nyingine “Waandishi wa Habari
Hewa”,wanaodhalilisha taaluma hii.
Lakini
pia hatutasita kuchukua hatua kwa waandishi wa habari wanaoshirikiana
na waandishi hewa kwa shughuli za kiuandishi wa habari.
Tunaahidi kushirikiana na vyombo vya dola katika kuhakikisha kuwa taaluma ya uandishi wa habari inaheshimika.
Imetolewa na
Kadama Malunde
Mwenyekiti SPC
11.05.2016
0 comments:
Post a Comment