Na Theresia Mwami TEMESA Shinyanga
Wakala
wa Ufundi na Umeme TEMESA Mkoa wa Shinyanga inazidai Halamashauri,
Mashirika na Taasisi za Serikali mkoani humo jumla ya shillingi
163,269,269.82 kutokana na kupata huduma ya matengenezo ya magari.
Katika
taarifa yake kwa Mtendaji Mkuu wa TEMESA, Meneja wa TEMESA Shinyanga
Mhandisi Riziki Lukali amesema madeni hayo ni ya mwaka wa fedha
2016/2017 na wamesha wasilisha madai yao kwa wahusika na wanasubiri
kulipwa.
Mhandisi Riziki Lukali aliwataja wadaiwa hao kuwa ni TANROADS Shinyanga Sh 24,193,733.21, TANESCO Shinyanga
Sh Milioni 96,267,987.63, DED Kishapu Sh 6,753,735.03, RAS Shinyanga Sh
2,742,097.36, KUWASA Kahama Sh 9,855,714, KASHUWASA Shinyanga Sh
1,992,430, TBA Shinyanga Sh 5,103,062.56, Mahakama Kuu Shinyanga Sh
5,470,628.91, Uhamiaji Shinyanga Sh 896,333.63, DAS Kishapu Sh
1,071,573.57, NSSF Shinyanga Sh3,798,184 pamoja na RMO Shinyanga
shilingi 5,123, 789.92 milioni na jumla ya madeni hayo yote ni Sh
163,269,269.82.
Kwa
upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt.
Mussa Mgwatu amefurahishwa na utaratibu wa TEMESA Shinyanga wa kuzuia
magari ya taasisi, halmashauri na mashirika yanayodaiwa na kituo hadi hapo yatakapolipiwa gharama za matengenezo.
Na
pia amemuagiza Meneja wa TEMESA Shinyanga kutoa taarifa kwake kama kuna
Taasisi za Serikali ambazo hukiuka Sheria kwa kutopeleka magari yake
kwenye karakana za TEMESA na kupeleka magari hayo kwenye karakana binafsi zilizomo mkoani humo ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa dhidi yao.
Dkt
Mgwatu amesisitiza watumishi kuendelea kujituma kufanya kazi kwa weledi
na kwa ubora zaidi ili karakana iweze kuvuta wateja wengi na kuongeza
pato la kituo.
Aidha
TEMESA Shinyanga kwa mwaka wa fedha wa 2016/2017 kituo kimepanga
kukusanya jumla ya Sh 458,160,000 kutokana na madeni na huduma
zinazoendelea kutolewa kituoni hapo.
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu yupo katika
ziara ya kutembelea vituo vya TEMESA vilivyopo Kanda ya Ziwa ili kubaini
changamoto mbali mbali zilizomo na kuzitafutia ufumbuzi.
0 comments:
Post a Comment