Home » » KAMATI YA FEDHA KISHAPU YAFANYA ZIARA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO

KAMATI YA FEDHA KISHAPU YAFANYA ZIARA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Boniphace Butondo akiongozana na
mchumi kutoka halmashauri hiyo, Veronica Massawe katika kukagua mradi wa ujenzi
wa vyumba vya madarasa.
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Boniphace Butondo akiwaelekeza
jambo mafundi waliokutwa na kamati wakiendelea na shughuli ya kusakafia mojawapo
ya vyumba vya madarasa.
Wajumbe wa Kamati ya Fedha, Ungozi na Mipango wakikagua mradi wa ujenzi wa
mojawapo ya vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Lagana wakati wa ziara
hiyo.
Ofisa elimu ufundi, Moshi Balele akiwaelekeza wajumbe wa kamati namna ujenzi wa
chumba cha darasa unavyoendelea katika shule ya msingi Ipililo.
Chumba cha darasa katika shule ya msingi Mwamadulu ata ya Lagana kikiwa katika
hatua mwisho wa ujenzi wake.


Na Robert Hokororo

Kamati ya Fedha, Ungozi na Mipango halmashauri ya wilaya ya Kishapu imefanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo kwenye kata za Lagana, Itilima na Talaga.

Katika ziara hiyo wajumbe hao pamoja na wataalamu kutoka halmashauri walitembelea maendeleo ya ukarabati wa vyumba viwili vya madarasa shule ya msingi Mwadulu
iliyopo kata ya Lagana.

Wakiwa eneo hilo wajumbe hao kupitia kwa mwenyekiti wa halmashauri, Boniphace Butondo walipongeza juhudi za uongozi wa shule hiyo kwa ubunifu na kutumia vizuri
fedha za Serikali.

Butondo aliwataka wanakamati ya shule kuendelea kuupa ushirikiano uongozi wa shule hiyo ili waendelee kushughulikia shughuli za maendeleo kupitia mpango wa elimu bure.

Kamati hiyo iliweza pia kukagua maendeleo ya ujenzi wa nyumba ya walimu katika shule ya msingi Lagana ambayo inajengwa kwa nguvu ya wananchi ambapo walihimiza
waendelee kuchangia.

Ziara hiyo pia ijumuisha kata ya Itilima ambapo wajumbe na wataalamu hao walikagua ujenzi wa vyumba viwili vya darasa shule ya msingi Ipililo pamoja na kata ya Talaga ukarabati wa vyumba vya madarasa shule ya msingi Nhobola.

Waliridhishwa na kasi ya maendeleo ya ujenzi huo ambapo walimpongeza afisa elimu ufundi, Moshi Balele kwa kufuatilia kwa ukaribu shughuli zote zinazoendelea.

Hiyo ni mojawapo ya ziara za kukagua miradi ya maendeleo zinazofanywa na kamati mbalimbali za Baraza la Madiwani katika halmashauri hiyo kwa lengo la kuboresha
maisha ya wananchi.


0 comments:

 
Supported by Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Shinyanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa