Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Kushoto ni Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu Graham Crew akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu hundi yenye thamani ya Shilingi milioni 460 kwa ajili ya ushuru wa Huduma kwa halmashauri ya Msalala.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu Graham Crew akizungumza wakati wa kukabidhi hundi yenye thamani ya Shilingi milioni 460 kwa ajili ya ushuru wa Huduma kwa halmashauri ya Msalala wilayani Kahama leo Jumatano Julai 26,2017 katika ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Kahama.Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu.
Hundi yenye thamani ya Shilingi milioni 460 iliyotolewa na Mgodi wa Acacia Bulyanhulu kwa ajili ya ushuru wa Huduma kwa halmashauri ya Msalala.
Kushoto ni Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu Graham Crew akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu hundi yenye thamani ya Shilingi milioni 460 kwa ajili ya ushuru wa Huduma kwa halmashauri ya Msalala.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu (kulia) akishikana mkono na Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu Graham Crew wakati wa zoezi la kukabidhi hundi yenye thamani ya Shilingi milioni 460 kwa ajili ya ushuru wa Huduma kwa halmashauri ya Msalala.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu akimkabidhi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala hundi yenye thamani ya Shilingi milioni 460 kwa ajili ya ushuru wa Huduma kwa halmashauri ya Msalala.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala Simon Berege akizungumza wakati akimkabidhi hundi hiyo Kaimu Mweka Hazina wa halmashauri hiyo Saleh Bugege (kushoto). Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano ya Jamii mgodi wa Acacia Bulyanhulu Sarah Ezra Terry.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala Simon Berege akizungumza baada ya kupokea hundi yenye thamani ya shilingi milioni 460 kwa ajili ya ushuru wa Huduma kwa halmashauri ya Msalala.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu akizungumza wakati wa makabidhiano ya hundi yenye thamani ya shilingi milioni 460 kwa ajili ya ushuru wa Huduma kwa halmashauri ya Msalala.
Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog
Mgodi
wa dhahabu wa Acacia Bulyanhulu (BGML) uliopo katika Halmashauri ya
Msalala wilaya ya Kahama mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Julai 26,2017
umekabidhi hundi yenye thamani ya Shilingi 460,732,841.08/= kwa ajili ya
ushuru wa Huduma kwa halmashauri ya Msalala.
Akizungumza
wakati wa kukabidhi hundi hiyo,Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu
Graham Crew alisema kiasi hicho ni asilimia 67 ya malipo ya ushuru wa
huduma kwa ajili ya kipindi cha miezi sita kuanzia Januari hadi mwezi
Juni mwaka huu ambacho ni asilimia 0.3 ya ukokotoaji wa ushuru wa huduma
wa mgodi huo katika kipindi hicho.
“Jumla
ya malipo ya ushuru wa huduma kwa kipindi cha miezi sita iliyopita ni
shilingi za Kitanzania 687,660,956.84/=,ambapo malipo hayo yamegawanywa
katika halmashauri mbili ambazo ni Msalala inayopata asilimia 67 na
Nyang’wale iliyopo mkoani Geita inapata asilimia 33”,alifafanua Crew.
Alisema
kutokana na mgawanyo huo,halmashauri ya Msalala imelipwa shilingi
milioni 460 (460,732,841.08/= ) na Nyang’wale shilingi Milioni 226
(226,928,115.76/=.
"Ushuru
umepungua kwa kuwa mgodi haujafanya mauzo ya makinikia ambayo yamezuiwa
tangu mwanzoni mwa mwezi machi mwaka huu, hivyo tunafahamu kuwa
tutalipa zaidi tutakapouza makinikia ambayo yapo yanaendelea kukusanywa
mgodini",aliongeza Crew.
Katika
hatua nyingine Crew alisema tangu mwaka 2000 mpaka sasa mgodi huo
umelipa zaidi ya shilingi 10,247,742,957/= za kodi ya ushuru wa huduma
na kampuni ya Acacia ilianza kutoa malipo ya ushuru wa huduma wa
asilimia 0.3 ya mapato ghafi kwa halmashauri husika mwaka 2014.
“Mgodi
wetu unaendelea kuwa na matarajio ya kuchangia kuimarisha sekta ya
viwanda kwenye uchimbaji madini katika halmashauri ya Msalala huku
tukiendelea kutekeleza mkakati wa Jamii Endelevu wa Acacia ulioanzishwa
mwaka 2016 kwa kushauriana na wadau lengo likiwa ni kuchangia maendeleo
ya Jamii Endelevu inayonufaika na kukua kwa uchumi ndani ya jamii ili
kujenga mahusiano ya kuaminika”,alisema Crew.
Akipokea
hundi hiyo kisha kuikabidhi kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala,
Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu aliushukuru mgodi wa Acacia
Bulyanhulu kwa kuendelea kuunga mkono jitihada za serikali katika kutoa
huduma kwa jami.
“Hiki
kiwango cha shilingi milioni 460 tulichopokea ni kiwango kizuri ingawa
kimepungua ulikinganisha na kipindi cha miezi sita cha Mwezi Juni hadi
Desemba 2016,furaha inatujaza kwamba ile shilingi milioni 300 na zaidi
ipo ndani ya Makinikia, yatakapouzwa tutaipata na tutaendelea kuboresha
huduma za kijamii”,alieleza Nkurlu.
Nkurulu
alimuomba mkurugenzi wa halmashauri ya Msalala kuhakikisha fedha
zilizotolewa na mgodi huo zitumike kwa huduma za kijamii kama
zilivyokusudiwa ikiwemo kuboresha huduma za afya na miundombinu.
Naye
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala Simon Berege alisema mapato
waliyopokea kutoka mgodi huo yako chini kwa shilingi milioni 300
ukilinganisha na kipindi kilichopita cha kuanzia Mwezi Julai hadi
Desemba 2016 ambapo mgodi huo ulipokea shilingi milioni 760.
“Sisi
tumepokea mapato haya kama tunavyopkea mapato mengine tunayopata katika
halmashauri zetu,mapato haya ni yako chini ukilinganisha na kipindi
kilichopita,tunaambiwa mapato yamepungua kutokana na Makinikia ambapo
sasa yamesimama,hii inaleta changamoto katika ukusanyaji wa mapato
katika halmashauri yetu, tunaamini mazungumzo baina Acacia na serikali
yakiisha halmashauri yetu itapata mapato mengi zaidi”,aliongeza Berege.
0 comments:
Post a Comment