Home » » MAKALA YA ELIMU: KISHAPU YAENDELEA KUBORESHA SEKTA YA ELIMU

MAKALA YA ELIMU: KISHAPU YAENDELEA KUBORESHA SEKTA YA ELIMU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga akimkabidhi msaada wa vifaa vya maabara, stuli za kukaliwa wanafunzi wakati wa mazoezi kwa vitendo kwa aliyekuwa mkuu wa shule ya sekondari Kishapu ambaye sasa ni mratibu elimu kata ya Sekebugora, mwalimu Hosea Somi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga akikagua mojawapo ya vyoo va nyumba za walimu katika shule ya sekondari Kiloleli kata ya Kiloleli wilayani humo.
Sehemu ya nyumba za walimu katika shule ya sekondari Kililoli kata ya Kiloleli wilayani humo ambazo ni mojawapo ya mpango wa halmashauri kuboresha sekta hiyo muhimu.

Na Robert Hokororo, Kishapu DC
Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga inaendelea na mkakati wake wa kuboresha mazingira ya sekta ya elimu kwa kujenga miundombinu katika shule zake mbalimbali. Inafanya hivyo kupitia programu mbalimbali zikwemo Mpango wa kuboresha Miundombinu katika shule za sekondari (SEDP) ili kumpa mwanafunzi mazingira mazuri ya kujifunza.

Pia halmashauri hiyo kupitia Idara ya Elimu Sekondari ina jukumu kubwa la kuhakikisha shule zake zinafanya vizuri katika mitihani ya kitaifa na hatimaye kuitoa kimasomaso wilaya kitaaluma. Imekuwa ikitekeleza miradi mbalimbali ikiwa na lengo la kupanua wigo wa elimu katika shule mbalimbali za sekondari na hivyo wanafunzi kuwa na mazingira mazuri ya kujifunza.

Wanafunzi wanapokuwa na mazingira mazuri ya elimu ikiwemo miundombinu rafiki kwao wanakuwa na ari ya kujifunza na hatimaye kufaulu. Vile vile walimu nao wanapokuwa na wamewekewa mazingira mazuri ya kufundishia huweza kufanya kazi kwa nguvu moja na kwa moyo wote. Miongoni mwa miradi hiyo ni ujenzi wa vyumba vya madarasa, nyumba za walimu, maabara na vyoo endapo vikiwa katika ubora vinakuwa motisha kubwa kwa walimu na wanafunzi.

0 comments:

 
Supported by Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Shinyanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa