Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Naibu
Meya wa Manispaa ya Shinyanga,Mheshimiwa Agnes Machiya akifungua kikao
maalum cha baraza la madiwani leo Ijumaa Septemba 29,2017.-Picha na
Kadama Malunde - Malunde1 blog.
Naibu Meya wa Manispaa hiyo,Agnes Machiya akizungumza wakati wa baraza la madiwani wa manispaa ya Shinyanga leo
Kaimu
Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga,Magedi Magenzi akizungumza katika
kikao maalum cha baraza la madiwani wa manispaa hiyo.
Mchumi
wa manispaa ya Shinyanga,Raymond Kilindo akiwasilisha taarifa ya miradi
ilizotekelezwa katika manispaa hiyo kwa mwaka wa 2016/2017 na taarifa
za hesabu za mwisho za halmashauri hiyo kwa mwaka wa fedha ulioishia
June 30,2017.
Diwani wa kata ya Lubaga,Mchungaji Obeid Jilala akiwa katika kikao hicho.
Madiwani wakiwa ukumbini.
Madiwani wakiwa katika kikao hicho.
Diwani wa kata ya Ndembezi David Nkulila akielezea uwalakini wake katika taarifa zilizowasilishwa kwenye kikao hicho.
Diwani
wa kata ya Kambarage,Hassan Mwendapole akichangia hoja ukumbini huku
akiitaka manispaa ya Shinyanga kuacha kuwa inaleta kwa dharura taarifa
zinazohusu masuala ya fedha.
Kikao kinaendelea.
Diwani wa kata ya Mwawaza,Juma Nkwambi akichangia hoja katika kikao hicho.
Kikao kinaendelea.
Madiwani wakiwa ukumbini.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Baraza
la madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga limepitisha taarifa
miradi zilizotekelezwa katika manispaa hiyo kwa mwaka wa 2016/2017 na
taarifa za hesabu za mwisho za halmashauri hiyo kwa mwaka wa fedha
ulioishia June 30,2017.
Taarifa
hizo zimepitishwa katika kiako maalum cha baraza la madiwani
kililofanyika leo Ijumaa Septemba 29,2017 katika ukumbi wa Lewis
Kalinjuna mjini Shinyanga.
Kaimu
Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga,Magedi Magenzi alisema baada ya
madiwani kupitisha taarifa hizo zitapelekwa kwa mkaguzi mkuu na
mdhibiti wa hesabu za serikali (CAG) na kamati za Bunge Hesabu za
serikali za Mitaa (LAAC).
Naibu
Meya wa Manispaa hiyo,Agnes Machiya aliwaomba madiwani kuendelea
kushirikiano na kushikamana ili kuwaletea maendeleo wananchi.
Hata
hivyo kabla ya taarifa hizo kupitishwa baadhi ya madiwani waliutaka
uongozi wa manispaa ya Shinyanga kuacha utaratibu wa kupeleka taarifa
zinazohusu masuala ya fedha kwa dharura kwani huenda kuna mapungufu
yanaweza kujitokeza matokeo yake madiwani kuonekana wamepitisha taarifa
zisizo sahihi.
"Hizi
taarifa nyeti za mwisho wa mwaka,zimekuja ghafla tu,kablasha kubwa kama
hili ni vigumu kulipitia mara moja,binafsi baada ya kujaribu kulipitia
nimebaini kuwepo na mashaka katika baadhi ya miradi,kunaubadhirifu wa
fedha",alieleza Diwani wa kata ya Ndembezi David Nkulila.
"Mwaka
jana pia mlileta taarifa nyeti kama hizi kwa dharura,Huu uwe mwanzo na
mwisho kuleta taarifa kama hizi kwa dharura",aliongeza diwani wa kata ya
Kambarage Hassan Mwendapole.
Kaimu
Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga,Magedi Magenzi alisema taarifa hizo
zimeletwa kwa dharura kutokana na taarifa hizo kuhitajika mahali
panapohusika.
0 comments:
Post a Comment