Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Afisa
mradi wa “Usawa wa kijinsia kiuchumi kwa wanawake na vijana" kutoka
Shirika la Kivulini lenye makao makuu yake jijini Mwanza, Eunice
Mayengela akizungumza wakati wa mafunzo ya usawa wa kijinsia,sera na
sheria zinazohusu usawa wa kijinsia kwa wadau wanaotekeleza mradi huo
leo katika ukumbi wa Empire Hotel Mjini Shinyanga-Picha na Kadama
Malunde - Malunde1 blog
Afisa
Mradi kutoka shirika la Oxfam,Mkamiti Mgawe akifungua mafunzo ya usawa
wa kijinsia,sera na sheria zinazohusu usawa wa kijinsia kwa wadau
wanaotekeleza mradi wa “Usawa wa kijinsia kiuchumi kwa wanawake na
vijana”.
Shirika la Kivulini limetoa mafunzo ya usawa wa kijinsia,sera na sheria
zinazohusu usawa wa kijinsia kwa wadau wanaotekeleza mradi wa “Usawa wa
kijinsia kiuchumi kwa wanawake na vijana” kutoka kata ya Nyida,Nsalala
na Itwangi katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Mradi huo unatekelezwa na Shirika la OXFAM kwa kushirikiana na shirika la Kivulini.
Mafunzo hayo ya siku moja yamefanyika leo Alhamis Septemba 28,2017 katika ukumbi wa Empire Hotel mjini Shinyanga.
Miongoni mwa wadau waliofaidika na mafunzo hayo ni maafisa maendeleo ya
jamii,maafisa watendaji wa vijiji na kata,viongozi wa mabaraza ya
kata,sungusungu,maafisa ustawi wa jamii,afya,wawakilishi kutoka dawati
la jinsia wilaya ya Shinyanga.
Awali akizungumza katika mafunzo hayo, Ofisa mradi kutoka Shirika la
Kivulini lenye makao makuu yake jijini Mwanza, Eunice Mayengela alisema
lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uelewa viongozi wa serikali za mitaa
kuhusu masuala ya usawa wa kijinsia,sera na sheria zinazohusu usawa wa
kijinsia.
“Tunatekeleza mradi wa “usawa wa kijinsia kiuchumi kwa wanawake na
vijana katika halmashauri ya wilaya ya Kishapu na Shinyanga Vijijini na
leo tumekutana na wadau kutoka kata tatu za Nyida,Nsalala na Itwangi za
Shinyanga Vijijini,lengo la mradi huu ni kujenga uwezo, uelewa na
mikakati ya kutoa elimu na kuhamasisha jamii kuzuia na kupambana na
ukatili wa kijinsia”,aliongeza Mayengela.
Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo,mgeni rasmi ambaye ni Afisa
Mradi kutoka shirika la Oxfam,Mkamiti Mgawe alisema mafunzo hayo
yatawasaidia wadau hao kutekeleza vyema majukumu yao katika kupinga na
kupambana na ukatili wa kijinsia kwenye maeneo yao.
“Mafunzo haya yanajumuisha viongozi wa serikali za mitaa ambako ndiko
matukio mengi ya ukatili wa kijinsia yanafanyika,tumieni elimu hii
kufikisha ujumbe kwa jamii kwamba ukatili wa kijinsia haukubaliki”,alisema Mgawe.
Alisema viongozi wa serikali za mitaa na maafisa ustawi wa jamii wana
jukumu la kuwashauri waathirika wa vitendo vya kikatili juu ya haki zao
kupeleka mashtaka ya ukatili katika vyombo vya usalama ikiwemo polisi na
mahakama.
Naye Mwezeshaji wa mafunzo hayo,Glory Mlaky alizitaja baadhi ya sababu
za ukatili katika jamii kuwa ni wanawake wengi kuamini kuwa wao ni
dhaifu,wanaohitaji kuongozwa,kuelekezwa na kuwajibishwa na wanaume
pamoja na wanawake hao kukosa elimu kuhusu haki zao.
Kwa upande wake,Kaimu Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii na Vijana
Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga vijijini,Deus Masili Muhoja aliwasihi
viongozi wa serikali za mitaa kuwaelimisha wananchi kuhusu masuala ya
ukatili wa kijinsia na kuwasisitiza wawe tayari kutoa ushahidi ili
waathirika wapate haki yao.
Afisa kutoka Jeshi la Polisi wilaya ya Shinyanga,Joseph Christopher
aliwataka viongozi wa jeshi la jadi sungusungu kuimarisha usalama katika
maeneo yao na wanapokamata mhalifu wamfikishe kituo cha polisi badala
ya kujichukulia sheria mkononi kumwadhibu.
Afisa Mradi kutoka shirika la Oxfam,Mkamiti Mgawe akifungua mafunzo ya
usawa wa kijinsia,sera na sheria zinazohusu usawa wa kijinsia
akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo.
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa ukumbini
Wadau wakifuatilia mafunzo
Afisa mradi wa kutoka Shirika la Kivulini,Eunice Mayengela akisisitiza jambo ukumbini.
Mafunzo yanaendelea....
Afisa mradi wa kutoka Shirika la Kivulini,Eunice Mayengela akizungumza ukumbini.
Mwezeshaji wa mafunzo hayo,Glory Mlaky akitoa elimu kuhusu masuala ya ukatili katika jamii.
Mwezeshaji wa mafunzo hayo,Glory Mlaky akielezea kuhusu ukatili wa kingono.
Bwana Beatu Berenardo kutoka kijiji cha Welezo kata ya Nsalala akichangia hoja ukumbini
Washiriki wa mafunzo wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini
Afisa Mtendaji wa kata ya Nyida Daudi Lazaro akichangia hoja wakati wa mafunzo hayo.
Mwezeshaji wa mafunzo hayo,Glory Mlaky akiendelea kutoa mada wakati wa mafunzo hayo.
Washiriki wa mafunzo wakifuatilia mada ukumbini
Mwenyekiti wa Baraza la ardhi kutoka kata ya Itwangi,Joseph Maganga akichangia hoja ukumbini
Washiriki wa mafunzo wakifanya kazi ya kundi
Kazi za makundi zinaendelea
Kazi ya kundi inaendelea
Afisa Maendeleo wa kata ya Nsalala,Beatrice Macha akiwasilisha kazi ya kundi lake
Katibu wa jeshi la sungusungu kata ya Nsalala John Machiya akiwasilisha kazi ya kundi lake
Washiriki wa mafunzo wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini
Mwakilishi wa Jeshi la Polisi wilaya ya Shinyanga,Joseph Christopher akizungumza ukumbini
Kaimu Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii na Vijana Halmashauri ya
wilaya ya Shinyanga vijijini, Deus Masili Muhoja akizungumza ukumbini
Picha ya pamoja washiriki wa mafunzo hayo.
Picha na Kadama Malunde - Malunde1 blog
0 comments:
Post a Comment