Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mbunge wa viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal (CCM) akikabidhi baiskeli kwa mwanafunzi mwenye ulemavu (hatembei wala haongei) katika shule ya msingi Tinde-Picha na Said Nassor-Malunde1 blog Tinde
Mbunge wa viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal (CCM) akikabidhi baiskeli kwa mwanafunzi mwenye ulemavu wa viungo katika shule ya msingi Tinde,aliyeshikilia kipaza sauti ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mheshimiwa Josephine Matiro.
Mbunge
wa viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal (CCM)
ametembelea shule ya msingi aliyosoma Tinde iliyopo katika kata ya Tinde
wilaya ya Shinyanga kisha kutoa msaada kwa wanafunzi nane wenye ulemavu
wa viungo akiwemo kijana ambaye hawezi kuongea wala kutembea. Mbunge huyo ametembelea shule hiyo jana Jumatano Septemba 27,2017.
Mheshimiwa
Hilal ametoa msaada wa baiskeli kwa kijana ambaye hawezi kutembea wala
kuongea anayesoma katika shule hiyo huku akijitolea kuwanunulia
wanafunzi hao nane mahitaji yao yote ya shule mpaka watakapomaliza
masomo yao ya shule ya msingi.
“Hii
shule nimesoma,baada ya kufika hapa nimeambiwa kuna watoto wenye
ulemavu,baada kumuona kijana huyu nimempatia baiskeli lakini pia
nimejitolea kuwahudumia wanafunzi hawa wanane ambao wana ulemavu wa
viungo,nitawanunulia mahitaji yao ya shule na watakuwa wanakunywa uji
kila siku kwa gharama zangu”,ameeleza Mbunge huyo.
Mbali
na kutoa msaada huo Mheshimiwa Azza Hilal ameshiriki zoezi la Upandaji
miti katika wilaya ya Shinyanga lililoanzishwa na Mkuu wa wilaya ya
Shinyanga Josephine Matiro lenye kauli mbiu ya "Shinyanga Mpya, Mti
Kwanza".
Akiwa
katika kata ya Tinde,mbunge huyo aliungana na mkuu wa wilaya ya
Shinyanga Josephine Matiro kupanda miti katika shule ya msingi Tinde,pia
katika barabara kuu ya kutoka Tinde kwenda Kahama na barabara ya kutoka
Tinde kwenda Nzega mkoani Tabora.
0 comments:
Post a Comment