Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro ametembelea vituo sita vya huduma ya mtoto katika makanisa ya kiinjili yaliyo na ushirika na Compassion International Tanzania Klasa ya Shinyanga yenye vituo tisa.
Mkuu huyo wa wilaya amefanya ziara hiyo leo Jumamosi Disemba 2,2017 kwa ajili ya kujionea stadi za maisha na miradi mbalimbali inayofanywa na watoto wanaopata huduma katika vituo hivyo.
Vituo vilivyotembelewa ni vituo vya Kanisa la ACT Shinyanga Mjini,AICT Kolandoto,TAG Shinyanga Mjini,PAG Shinyanga Mjini,KKKT Shinyanga Mjini.
Akiwa katika ziara hiyo,Matiro amejionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na watoto kama vile utengenezaji skonzi,biskuti,keki,nguo,mafuta,sabuni pamoja na ususi,ufumaji,saluni,ufyatuaji wa matofali,uchomeleaji wa vyuma,useremala,masomo ya kompyuta na mambo mengine kadha wa kadha.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo,mkuu huyo wa wilaya alilipongeza shirika la Compassion kupitia makanisa yanayosimamia vituo hivyo ambavyo vimekuwa msaada mkubwa kwa watoto ambao wanajengewa uwezo wa kujiajiri.
“Nimegundua tuna jeshi kubwa la vijana wenye ujuzi wa aina mbalimbali,vijana tumieni fursa hii ya Compassion kujinufaisha kwa ajili ya maisha yenu,sisi kama serikali tunafarijika sana kuona vijana wakijengewa uwezo wa kujiajiri ili kuleta maendeleo katika jamii”,alieleza.
Matiro alieleza kufurahishwa kuona jinsi vijana hao wanavyojengewa uwezo wa kutengeneza bidhaa mbalimbali na kuwashauri kuongeza jitihada ili kutengeneza viwanda kamili vya kutengeneza bidhaa.
“Sera ya serikali ni kuwa na viwanda,nimeona vijana wanatengeneza skonzi,biskuti kwa kutumia mashine za kisasa kabisa katika kituo cha AICT Ngokolo,hiki ni kiwanda,naomba kanisa na Compassion kwa kushirikiana na serikali tuangalie namna ya kupanua kiwanda hiki ili kuleta mabadiliko katika jamii na kitasaidia vijana kujikwamua kiuchumi”,alisema Matiro.
Katika hatua nyingine aliwataka wahusika katika vituo hivyo kuhakikisha msaada unaotolewa na shirika hilo kuwafikia watoto wanaolengwa huku akiwataka kushirikiana kwa ukaribu na viongozi wa serikaliza mitaa ili kubaini watoto wanaohitaji msaada kutokana na ugumu wa maisha.
Awali akisoma taarifa kuhusu vituo vya huduma ya mtoto katika klasta ya Shinyanga,Katibu wa wachungaji klasta ya Shinyanga,Askofu Thomas Faida alisema shirika la Compassion linahudumia watoto 2,110 wanaoishi kwenye mazingira magumu katika manispaa ya Shinyanga.
Alisema watoto hao hupatiwa misaada mbalimbali kama vile kufundishwa stadi za maisha,kupewa elimu ya ujasiriamali,kupewa sare za shule,madaftari,nguo,ada ya shule,gharama za matibabu na mambo mengine kadhaa.
Kwa upande wake Msimamizi wa vituo vya huduma ya mtoto klasta ya Kanda ya ziwa,Emmanuel Pando alisema shirika la Compassion linafanya shughuli zake kwa ushirika wenza na makanisa katika kuwahudumia watoto walioko katika mazingira magumu.
Pando alisema shirika hilo litaendelea kushirikiana na serikali ili kufanikisha mambo mbalimbali ambayo serikali inataka yafanikiwe.
ANGALIA PICHA ZA MATUKIO WAKATI WA ZIARA YA MKUU WA WILAYA YA SHINYANGA KATIKA VITUO 6 VYA HUDUMA YA MTOTO
Mwenyekiti wa Wachungaji klasta ya Shinyanga,Askofu Josephat Masaga kutoka kanisa la TAG Shinyanga akimpokea mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro katika kituo cha kanisa la ACT Shinyanga mjini kwa ajili ya kutembelea stadi za maisha na miradi inayofanywa na watoto katika kituo hicho.
Mkurugenzi wa kituo cha huduma ya watoto kanisa la ACT Shinyanga Mjini,Hagai Daniel akimwongoza mkuu wa wilaya ya Shinyanga kwenda kuangalia stadi za maisha na miradi inayofanywa na watoto wanaohudumiwa katika kituo hicho.
Vijana wakimuonesha mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro keki walizotengeneza.Vijana hao walisema wamepatiwa ujuzi wa kutengeneza keki katika kituo hicho.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiangalia jinsi wanavyochomelea vyuma katika kituo cha kanisa la ACT Shinyanga mjini.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwa katika chumba cha ufumaji katika kituo cha kanisa la ACT Shinyanga mjini.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwa katika chumba kwa ajili ya mambo ya ususi.Vijana wanaendelea kusukana.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akipokelewa katika kituo cha Kanisa la AICT Kolandoto. Wa kwanza kulia ni diwani wa kata ya Kolandoto,Agnes Machiya,ambaye ni pia ni naibu meya wa manispaa ya Shinyanga.Katikati ni Mchungaji Kiongozi kanisa la AICT Kolandoto,Jacob Osora
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwa katika chumba cha Kompyuta katika kituo cha AICT Kolandoto.Kulia ni mwalimu wa Kompyuta katika kituo hicho, Lucas Masaba.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akipanda mti wa kumbukumbu katika kituo cha AICT Kolandoto.
Watoto katika kituo cha AICT Kolandoto wakiimba wimbo
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiangalia jinsi watoto wanavyotumia kompyuta katika chumba cha kujifunzia Kompyuta katika kituo cha AICT Ngokolo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akimwangilia kijana akishona nguo kwa kutumia cherehani katika kituo cha AICT Ngokolo
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiangalia mashine zinazotumika kutengeneza skonzi na biskuti katika kituo cha AICT Ngokolo. Mkuu huyo wa wilaya alisema hicho ni kiwanda hivyo kinachotakiwa ni kuangalia namna ya kukipanua ili kilete maendeleo.
Mmoja wa vijana wanaotekeleza mradi wa kutengeneza skonzi na biskuti katika kituo cha AICT Ngokolo akionesha moja ya mitambo waliyonayo katika kituo hicho.
Kijana James Emmanuel akionesha mtambo wa kupasulia mbao katika kituo cha AICT Ngokolo.Alisema huwa wanatengeneza samani mbalimbali kama vile stuli,viti na vitanda.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akisalimia watoto katika kanisa la AICT Ngokolo
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwa amevaa mkoba uliotengenezwa kwa vitambaa laini katika kituo cha kanisa la TAG Shinyanga Mjini.
Kijana Rebeca Jeremiah akimuonesha mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro,moja ya vitambaa laini kwa ajili ya wanawake kujistiri wakiwa katika hedhi 'Pad' ambazo amekuwa akizitengeneza na kuziuza.Rebeca alisema pedi hizo unaweza kuzifua
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiangalia pedi ambayo unaweza kuifua na kuitumia mara nyingi.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akimpongeza Rebeca kwa ubunifu wa kutengeneza pedi.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro na msafara wake wakiwa katika kanisa la PAG Kambarage wakisalimiana na watoto
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiangalia bidhaa mbalimbali zinazotengezwa na watoto katika kituo cha kanisa la KKKT Shinyanga mjini.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akisikiliza maelezo kutoka kwa watoto kuhusu namna wanavyotengeneza sabuni kwa ajili ya matumizi mbalimbali ya nyumbani na ofisini.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza wakati akiangalia mitambo ya umeme iliyotengenezwa na watoto katika kituo cha KKKT Shinyanga mjini
Hapa ni katika ukumbi wa kanisa la KKKT usharika wa Ebenezer kanisa kuu Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria: Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza wa kikao cha majumuisho ya ziara yake kutembelea vituo vya huduma ya mtoto katika makanisa ya kiinjili yaliyo na ushirika na Compassion International Tanzania Klasa ya Shinyanga.
.
Katibu wa wachungaji klasta ya Shinyanga,Askofu Thomas Faida akizungumza katika kikao cha majumuisho ya ziara ya mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro kutembelea vituo vya huduma ya mtoto katika makanisa ya kiinjili yaliyo na ushirika na Compassion International Tanzania Klasa ya Shinyanga.
Msimamizi wa vituo vya huduma ya mtoto klasta ya Kanda ya ziwa,Emmanuel Pando akizungumza katika kikao hicho.
Katibu Mkuu wa kanisa la KKKT usharika wa Ebenezer kanisa kuu Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria,Happiness Gefi akizungumza wakati wa kikao cha majumuisho ya ziara ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro kutembelea vituo vya huduma ya mtoto katika makanisa ya kiinjili yaliyo na ushirika na Compassion International Tanzania Klasa ya Shinyanga.
Mwenyekiti wa Wachungaji klasta ya Shinyanga,Askofu Josephat Masaga kutoka kanisa la TAG Shinyanga akizungumza wakati wa kikao cha kikao cha majumuisho ya ziara ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro kutembelea vituo vya huduma ya mtoto katika makanisa ya kiinjili yaliyo na ushirika na Compassion International Tanzania Klasa ya Shinyanga.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
0 comments:
Post a Comment