Home » » Viwango vipya leseni za madini kikwazo

Viwango vipya leseni za madini kikwazo


na David Frank, Shinyanga
WAFANYABIASHARA wa madini ya dhahabu katika mikoa ya Shinyanga na Tabora, wameiomba serikali kupunguza viwango vya malipo ya leseni za ununuzi wa madini hayo kwani unatishia mustakabali wao kibiashara.
Wafanyabiashara hao walitoa kilio chao juzi mjini hapa mbele ya viongozi wa kitaifa wa Chama cha Wanunuzi na Wauzaji Madini nchini (TAMIDA).
Walisema kiwango cha ada ya leseni kwa wazawa imepanda kutoka sh 250,000 hadi milioni moja kwa mwaka, hali inayowafanya kushidwa kumudu gharama hizo.
Mmoja wa wafanyabiashara hao, Joseph Temela, alisema wengi wameshidwa kumudu kiwango hicho na gharama mbalimbali za maisha na kuiomba serikali kuangalia upya viwango hivyo.
“Kwa kweli wengi wa wafanyabiashara ni wale tunaoitwa walalahoi na mitaji yetu ni midogo, kupanda kwa ada hiyo ni kutuuwa sisi na familia zetu. Tunaiomba serikali itupunguzie…tunatambua serikali yetu ni sikivu itatusadia,” alisema Temela.
Naye Mwenyekiti wa TAMIDA nchini, Sammy Mollel aliwaeleza wafanyabiashara hao wataangalia jinsi ya kutoa mapendekezo kwa serikali katika kuimarisha na kukuza biashara hiyo kwa wazawa, ili kukuza ununuzi wa madini na kuongeza thamani na hatimaye uuzaji wake nje ya nchi uliongezee taifa pato.
Chanzo: Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Shinyanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa