Home » » AJALI YAUA MMOJA NA KUJERUHI 42 KAHAMA

AJALI YAUA MMOJA NA KUJERUHI 42 KAHAMA

Shija Felician, Kahama

MTU mmoja ambaye ni raia wa Rwanda amefariki dunia hapo hapo na wengine 42 kujeruhiwa katika ajali iliyotokea leo alfajiri mjinii Kahama baada ya gari la abiria la Kampuni ya Leina Tours lenye namba za usajili T 391 BWP kuanguka mita chache kutoka stendi kuu ya wilaya ya Kahama.
 
Katika ajali hiyo Mganga Mkuu wa wilaya ya Kahama, Dr.Emmanuel Andrew amesema mwili wa marehemu ambaye hakuweza kufahamika jina lake umehifadhiwa katika chumba cha maiti katika hospitali ya wilaya ya Kahama.
 
Dr.Andrew amesema katika ajali hiyo majeruhi 15 kati ya 42 wameruhusiwa baada ya kupatiwa hudumaya kwanza na wanne kati ya hao ni raia wa nchi ya Rwanda.
 
Mganga huyo amesema majeruhi waliobaki wanaendelea kupatiwa matibabu akiwemo dreva wa basi hilo Kayumba Yusuph [52]  na raia watatu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na saba kutoka nchini Rwanda huku dreva wa pikipiki Wilison Paschal [24] mkazi wa Nyahanga mjini Kahama ambaye alisababisha ajali hiyo hali yake ni mbaya.
 
Blogzamikoa

0 comments:

 
Supported by Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Shinyanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa