Mwandishi wetu, Kahama-Shinyanga Yetu
JUMLA ya Madiwani Ishirini na Tano kati ya Thelathini na mbili wanaounda Halmashauri ya Mji wa Kahama wameondoka jana kuelekea mjini Dodoma kwa mwaliko wa Mbunge wa Jimbo la Kahama, James Lembeli ambapo leo wamehudhuria vikao vya Bunge kushuhudia uwasilishwaji wa Bajeti ya Matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Kahama, bwana Machibya Jiduramabambasi amesema ziara hiyo pamoja na mwaliko wa Mbunge huyo ina lengo la kujifunza kutokana na upya wake kwakuwa tangu ianzishwe ni takribani mwezi mmoja tu uliomaliika.
Bwana Jiduramabambasi amesema mara tu baadaya kuamalizika kwa bajeti hiyo watarudi na tayari watakuwa wamepata upeo kwa vitendo namna ya uwasilishaji wa Bajeti za Serikali.
Bajeti hiyo ya Wizara ya Maliasili na Utalii ambayo mwenyekiti wake ni mbunge huyo wa jimbo la Kahama, James Lembeli ambaye atawasilisha taarifa ya Kamati yake mbele ya madiwani wake hao aliowaalika kwenda Bungeni kujifunza.
Blogzamikoa
0 comments:
Post a Comment