Na Isaack Mbwaga, Maswa
Jumla ya mizani 233 ya kupimia uzito wa pamba na mbegu katika wilaya za maswa na meatu imekaguliwa na maafisa wa vipimo katika mkoa wa shinyanga katika oparesheni maalumu ya kuhakikisha wakulima hawapunjwi wakati wa kuuza pamba yao.
Meneja wa Vipimo katika Mkoa wa Shinyanga Luppi Shirima alisema kati ya mizani hiyo aina rula, 155 baada ya kugaliwa zimekutwa ziko katika vipimo sahihi na kuruhusiwa kuendelea na kazi wakati mizani 78 imekutwa imeharibiwa na watumishi wa makampuni yanayo nunua pamba kwa makusudi kwa lengo la kuwaibia wakulima wanapo uza pamba yao gulio
Shirima alisema mizani hizo zilikutwa zina wapunja wakulima kati ya kilo 12 hadi kilo 30 wakati wa kuuza pamba yao katika gulio
Meneja huyo alisema watu wote waliobainika kwa hujuma hiyo ya kuhujumu mizani ya kupimia pamba wametozwa faini kati ya shilingi 200,000/hadi 400,000/ kwa kila mizani iliyo kutwa imechakachuliwa
Hata hivyo alitoa onyo kwa watu wanaoharibu mizani kwa makusudi sheria itachukua mkondo wake kwa wenye makampuni.
Serikali ilitoa maelekezo kwa makampuni yote yanayo nunua pamba mwaka huu kutumia mizani aina ya dijitali katika kupimia pamba katika vituo wakati wa kunua pamba katika vituo hivyo.
Blogzamikoa
0 comments:
Post a Comment