Home » » MADIWANI WAJIPANGA KUMKATAA MKURUGENZI

MADIWANI WAJIPANGA KUMKATAA MKURUGENZI

na Ali Lityawi, Kahama
SIKU chache baada ya serikali kufanya mabadiliko ya wakurugenzi wa halmashauri, madiwani wilayani Kahama wameweka mikakati ya kumkataa mkurugenzi mpya kwa madai alishindwa uwajibikaji atokako kiasi cha kuisababishia hasara halmashauri yake.
Mkurugenzi huyo mpya ni Erika Msika aliyehamishiwa Kahama akitokea Sengerema mkoani Mwanza ambako anadaiwa alisimamishwa kazi kupisha uchunguzi pamoja na wakuu wake wa idara wa tuhuma ya ubadhirifu wa fedha za serikali zaidi ya sh bilioni sita.
Hali ya madiwani kumkataa mkurugenzi huyo ilianza kubainika wiki iliyopita baada ya Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Hawa Ghasia, kutangaza kufanya mabadiliko ya wakurugenzi wa halmashauri za wilaya, miji na manispaa ambapo sita walifukuzwa kazi na wengine wapya 14 kuteuliwa.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Kahama, Machibya Jidulamabambasi, alipotakiwa kuzungumzia hilo alikiri madiwani hao kujipanga kumkataa mkurugenzi huyo kutokana na kumshinikiza kuitisha kikao cha dharura cha baraza la madiwani.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Injinia Evarist Ndikilo, alipotakiwa kutoa ufafanuzi juu ya suala la mkurugenzi huyo kurudishwa kazini, alisema baada ya tume iliyoundwa kumaliza kazi yake alibainika hakuwa na hatia.
Chanzo: Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Shinyanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa