Mwandishi wetu, Kahama
TUME ya mabadiliko ya Katiba imetakiwa kuondoa kipengere cha Wanasiasa kuwa na sifa ya kujua kusoma na kuandika na badala yake kuwa na elimu ya Chuo Kikuu ambayo itakwenda sambamba na mabadiliko ya sayansi na teknoloji iliyopo sasa.
Changamoto hiyo imetolewa leo mjini Kahama wakati wa majadiriano ya kukusanya maoni juu ya uundaji wa Katiba mpya katika mdahalo ulioandaliwa na Mtandao wa Mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali wilayani Kahama.
Katika majadiliano hayo wananchi hao wamedai kumpa nafasi mgombea Ubunge ama Udiwani kuwa na sifa ya kujua kusoma na kuandika imepitwa na wakati kwa kuwa Taifa la sasa ni la wasomi ambalo haliwezi kuongozwa na viongozi wenye elimu ya namna hiyo.
Mmoja wa waongozaji katika mdahalo huo bwana Reuben Fanuel amesema katiba ya zamani imepitwa na wakati na iliandaliwa na watu wachache kwa lengo la kulinda utawala uliokuwapo madarakani.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa wilaya ya Kahama, bwana Ernest Masanja wakati akifungua mdahalo huo aliwataka wananchi wachangie kwa mawazo yako ili kuifanya Katiba mpya iwe na maslahi ya Kitaifa itakayowanufaisha watanzania wote.
Blogzamikoa
0 comments:
Post a Comment