na Stella Ibengwe, Shinyanga
WAHAMIAJI
haramu 11 raia wa Ethiopia wanashikiliwa na Idara ya Uhamiaji mkoani Shinyanga
kwa kosa la kuingia nchini kinyemela.
Raia
hao walikamatwa jana wakiwa ndani ya mabasi tofauti wakitokea jijini Mwanza na
kudai wanaelekea Tabora kwa ndugu zao.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana, Kaimu Ofisa Uhamiaji wa Mkoa, Salumu Farahani,
alithibitisha kukamatwa kwa raia hao na kueleza kuwa walikamatwa kwa nyakati
tofauti wakiwa ndani ya mabasi mawili tofauti, likiwa basi la AM Coach
linalofanya safari zake kati ya Mwanza na Tabora.
“Septemba
21 tuliwakamata raia nane na Septemba 23, tuliwakamata watatu na katika
mahojiano wanaeleza kuwa wanakwenda kwa ndugu yao aliyeko Tabora na mpaka sasa
tuna namba zake, lakini tukipiga simu yake haipatikani na wao wamekuwa sio
wakweli kueleza kile kinachowapeleka huko,” alisema.
Aliwataja
waliokamatwa kwenye basi la AM Coach kuwa ni Datun Suyubu, Tarkega Wadedebo na
Teshal Heliso na wengine Bahiradia Ibrahimu, Hand Chafario, Muktar Nuriya, Tofke
Gabir, Gatachawe Abute Chamso Hasawe, Tasfay Ayie na Muhba Gamali waliokamatwa
kwenye basi lingine.
Alisema
mbinu wanayoitumia kwa sasa wahamiaji hao ni kujiweka katika makundi madogo
madogo na sio makubwa kama ilivyozoeleka na kupanda mabasi, ili kukutana sehemu
ambayo wamepanga.
Chanzo: Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment