Na Patrick Mabula, Kahama
KATIKA hali ya isiyo ya kawaida Bundi wawili wameingia kwenye ukumbi wa
mikutano kisha kutua meza kuu wakati wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM), wilayani Kahama uliofanyika Shule ya Msingi Rocken Hill.
Kituko hicho kilitokea jana wakati ndege hao aina ya bundi walipotua katika
meza waliyokaa Mbunge wa Jimbo la Kahama, Bw.James Lembeli na Mwenyekiti wa CCM
Mkoa wa Shinyanga Bw.Hamis Mgeja.
Mbali na kutua kwenye za watu hao ambao ni mahasimu kisiasa, pia waliendelea
kukaa ukumbimbi wakati shughuli za uchaguzi zikiendelea hali iliyozusha hofu
miongoni mwa wajumbe wa mkutano huo.
Shuhuda wetu alieleleza kuwa tukio hilo lilitokea wakati wajumbe wakijiandaa
kuchagua viongozi wao, ndipo bundi ha wawili wawili waliingia kwenye ukumbi wa
mikutano. Kitendo cha bundi hao kuvamia mkutano huo kiliwafanya wajumbe
kutaharuki na kila mmoja akitafasiri tukio hilo kwa mtazamo wake na
wengine kulihusisha na imani za ushirikana.
Wakati wajumbe wakiwa wamekaa ukumbini ghafla bundi hao waliingia ukumbini na
kisha waliruka hadi kwenye meza ya Bw. Lembeli na Bw. Mgeja, kisha kusababisha matafaruku
mkubwa kwa wagombea nafasi mbali mbali.
Diwani wa Kata ya Chambo Bw.Damas Joseph, alisema mambo hayo
yanayodhaniwa kuwa ya kishirikina katika chaguzi za CCM ni lazima
yakemewe kwa vile yanawapa hofu mbalimbali na kuwafanya baadhi kutojiamini .
Bw. Deo Ndimila tangu Kata ya Ukune alithibitisha vitendo vya kishirikina
katika chaguzi za CCM mara nyingi zimekuwa zikitawala kwa baadhi ya watu
kuendekeza imani hizo potofu.
Chanzo: Majira
0 comments:
Post a Comment