JESHI la Polisi limeshauriwa kuchukua hatua za kumfikisha mahakamani
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman
Mbowe, akathibitishe ushahidi alionao kuhusu tuhuma alizoibua dhidi ya
Jeshi hilo kwamba linahusika katika tukio la mlipuko wa bomu uliotokea
hivi karibuni mkoani Arusha.
Ushauri huo ulitolewa mjini hapa juzi na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Shinyanga, Khamis Mgeja, alipowahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Ufala, Kata ya Kilago.
Alisema kitendo cha Mbowe kukataa kukabidhi ushahidi anaodai kuwanao ukimuonyesha mtuhumiwa wa tukio la ulipuaji bomu katika Viwanja vya Soweto mkoani Arusha, uliosababisha vifo vya watu watatu akishinikiza kuutoa hadi pale Rais Jakaya Kikwete atakapokuwa ameunda tume huru.
Alisema Mbowe anapaswa kufikishwa mahakamani mara moja ukweli upatikane, kwa kuwa yeye ndiyo anawajua wahusika.
Alisema fedha iliyoahidiwa na Paul Chagonja ni vizuri sasa kama haina kazi nyingine ielekezwe katika huduma za kijamii kama vile kununua dawa za hospitali au zikatengeneze madawati ya watoto katika shule za msingi na sekondari.
Aliwatahadharisha Watanzania kuwa makini na vyama vya upinzani, hususan CHADEMA kwa kuwa kinaendeshwa kwa misingi ya ushirikina wa kimataifa, yaani Freemasons, ambao msingi wao ni kutoa kafara na umwagaji wa damu.
“Hebu angalieni rangi ya bendera ya CHADEMA, ina rangi nyekundu lakini pia alama ya vidole viwili ni ishara ya watu wa freemason, hivyo tusipokuwa makini tutaendelea kumwaga damu,” alisema Mgeja.
Chanzo: Mtanzania

0 comments:
Post a Comment