Na Joachim Mushi, Aliyekuwa Kishapu
MBUNGE wa
Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jimbo la Kishapu mkoani Shinyanga, Seleiman
Nchambi amewaomba wapiga kura wake kuwa wavumilivu juu ya ahadi ya
huduma za maji safi na salama alizozitoa wakati akigombea jimbo hilo
katika uchaguzi mkuu 2010.
Nchambi
ametoa kauli hiyo hivi karibuni akizungumza na mwandishi wa habari hizi
kutoa ufafanuzi juu ya malalamiko ya baadhi ya wapigakura wake wa Kata
ya Kishapu, ambao wamelalamikia kitendo cha kuendelea kutopata huduma za
maji safi na salama eneo lao ilhali mbunge wao aliwaahidi kuwapatia
huduma hiyo.
Mbunge huyo alikiri kutoa ahadi ya huduma ya maji jimbo zima la Kishapu na utekelezaji wa ahadi zake unaenda awamu kwa awamu kama alivyopanga. Akifafanua zaidi alisema aliingia madarakani na kukuta sehemu kubwa ya jimbo hilo halina huduma ya maji safi na salama, lakini kwa jitihada zake mpaka sasa tayari amefanikiwa baadhi ya vijiji kuvipatia maji.
“Niliahidi
maji jimbo zima la Kishapu yaani jumla ya vijiji 114, wakati naingia
madarakani nimekuta hali ni mbaya ya huduma za maji…lakini hadi sasa
tunapozungumza zaidi ya vijiji 30 vinapata maji safi na salama huku
jitihada zingine zinaendelea,” alisema Nchambi akifafanua juu ya kilio
cha huduma za maji akizungumza kwa njia ya simu.
“Ahadi
yangu mimi ni miaka mitano, ilani ya CCM ni ya miaka mitano, ninaenda
kwa awamu yaani vijijini 10 kwa kila mwaka kwa wilaya,” aliongeza kusema
mbunge huyo.
Awali
uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa habari hizi kwa baadhi ya vijiji
vya Kata ya Kishapu, mkoani Shinyanga, vikiwemo vijiji vya Lubaga,
Isoso, Mwanuru pamoja na Kishapu ulibaini kuwepo na shida kubwa ya
huduma ya maji safi na salama hali inayowalazimu wananchi kutembea
umbali mrefu hasa kipindi cha kiangazi kutafuta maji.
Hata hivyo uchunguzi ulibaini mzigo mkubwa wa kukosekana kwa huduma ya maji safi na salama katika familia unawaangukia wanawake na wanafunzi ambao hutumia muda mrefu kusaka maji kwa ajili ya matumizi ya familia. Chanzo pekee cha maji ambacho hutegemewa na maeneo mengi ya vijiji ni cha Mto Tungu ambao nao hukauka kipindi cha kiangazi na wananchi kuendelea kupata maji kwa shida.
Hata hivyo uchunguzi ulibaini mzigo mkubwa wa kukosekana kwa huduma ya maji safi na salama katika familia unawaangukia wanawake na wanafunzi ambao hutumia muda mrefu kusaka maji kwa ajili ya matumizi ya familia. Chanzo pekee cha maji ambacho hutegemewa na maeneo mengi ya vijiji ni cha Mto Tungu ambao nao hukauka kipindi cha kiangazi na wananchi kuendelea kupata maji kwa shida.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti hivi karibuni viongozi wa vijiji vya Lubaga, Isoso,
Mwanuru na Kishapu walilalamikia kitendo cha wao kuendelea kuteseka kwa
huduma za maji ilhali walipewa ahadi ya kuletewa huduma hiyo na mbunge
wao kipindi cha kampeni.
Ofisa
Mtendaji wa Kijiji cha Lubaga, Enock Manyenye Shimba alisema mwaka 2010
wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu kijiji chao kilipewa ahadi ya
kuchimbiwa visima virefu vya maji na Mbunge wa Jimbo la Kishapu,
Seleiman Nchambi lakini anashangaa ahadi hiyo haijatekelezwa hadi leo.
Naye
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kishapu, George Kessy alikiri hali
mbaya ya huduma ya maji Wilaya nzima ya Kishapu kutokana na eneo hilo
kutokuwa na chanzo cha maji cha uhakika. Hata hivyo alisema juhudu
zinafanywa kuhakikisha uongozi unaondoa kero hiyo ya huduma ya maji kwa
wananchi.
“Ni kweli suala la maji ni Tatizo kwa wilaya nzima ya Kishapu, tena ni kubwa sana…,” alisema Kessy.
“Ni kweli suala la maji ni Tatizo kwa wilaya nzima ya Kishapu, tena ni kubwa sana…,” alisema Kessy.
Short URL: http://www.thehabari.com/?p=35464
0 comments:
Post a Comment