Na Thehabari.com, Kishapu
WASUKUMA
ni moja ya makabila nchini Tanzania ambayo awali yalishikilia desturi
ya familia kuwa na idadi kubwa ya watoto. Familia moja yaani baba na
mama waliendelea kuzaa kadri walivyo jaaliwa kupata watoto bila kujali
ukubwa wa familia. Mume pia hakuwa na kizuizi katika familia cha
kuongeza mke mwingine endapo atakuwa na ardhi (mashamba) na mifugo
(hasa ng'ombe) ya kutosha kuweza kuihudumia familia aliyonayo.
Wapo
walioamini kwamba kuwa na ukubwa wa familia ni kuongeza nguvu kazi
katika uzalishaji kwa kutumia ukubwa wa familia. Hata hivyo pia wapo
walioamini uzazi ni mpangilio wa Mungu hivyo haupaswi kupangiliwa na
wazazi bali mola mwenyewe. Hivyo basi familia za imani hii ziliendelea
kuza hadi pale uwezo wa kupata watoto ulipopotea wenyewe au vizuizi
vingine.
Hata
hivyo sasa hivi mambo yamebadilika kiuchumi, hali ni ngumu hivyo
familia nyingi zinapangia idadi ya watoto. Waliojisahau na kuendelea
kuzaa idadi kubwa ya watoto pasipo na uwezo kuwamudu wanajuta na
kutamani wangelipata uelewa wa elimu hiyo awali.
Hali
hii ya majuto ndiyo inayozikuta baadhi ya familia katika vijiji anuai
Kata ya Kishapu, mkoani Shinyanga, baada ya kuzungumza na mwandishi wa
makala haya. Familia hizi zimejikuta na idadi kubwa ya watoto kiasi cha
baba na mama kushindwa kuwapatia mahitaji ya msingi watoto wao hivyo
familia kuendelea kuwa na maisha duni kiuchumi.
Bi.
Rejina Moshwa (37) mkazi wa Kijiji cha Isoso ni miongoni mwa familia
zinazojutia uamuzi wa kuwa na idadi kubwa ya watoto. Anasema familia
yao ilikuwa na jumla ya watoto 10, lakini bahati mbaya wawili walifariki
dunia hivyo kubakia na watoto nane ambao ni mzigo mkubwa hivi sasa.
0 comments:
Post a Comment